246 ONLINE
246
246 Admin
Mwandishi — 246 ONLINE
Agosti 13, 2026
MADE BY GOOGLE 2026

 🚨 MADE BY GOOGLE 2026: Google Amepeleka Pixel Kwenye Level Nyingine — Gemini, Camera, Sign Language, Team Pixel na Mambo Mengi!

Kuanzia karibu saa 1:00 usiku, nilikuwa nimekaa macho  nikishuhudia Made by Google iliyoanza mpaka kuisha, na kwa sababu nilijua kuna vitu vipya vinakuja ilibidi ku-ON notification ya Made by Google —na nilitaka wana 246 ONLINE wasipitwe na chochote.

Lakini ukweli ni huu:

Google hakutoka tu na Pixel mpya.

Walionyesha namna wanavyotaka simu, AI, smartwatch, camera na hata vifaa vingine vya Google vifanye kazi pamoja.

Na baadhi ya demonstrations zilizofanyika kwenye stage zilinifanya nikae hivi:

“Subiri… AI imefanya nini hapo?” 😳

Kutoka kwa Gemini kuelewa unachomaanisha hata unapojisahihisha, kutafsiri lugha, kutambua American Sign Language (ASL) kupitia camera, kusaidia kupanga jibu kwa kutumia calendar yako, hadi Pixel 11 Pro kutumika kurekodi performance ya mwisho ya PinkPantheress...

Made by Google 2026 ilikuwa moto.

Na hapa 246 ONLINE tumekusanya mambo makubwa yaliyotokea.

Google Pixel 11 na Gemini Intelligence wakati wa Made by Google 2026: 246 Online


🎬 Trevor Noah Alifungua Show — Na Google Wakaanza Safari

Made by Google 2026 ilifunguliwa na Trevor Noah, ambaye alikuwa host wa event kutoka New York.

Alianza kwa utani kuhusu baadhi ya features mpya na akaeleza pia jinsi alivyopata nafasi hiyo baada ya kuwa akiacha comments kwenye video za Google za YouTube kupata chance sio mchezo eti 😁.

Na tangu mwanzo Google ikaweka wazi kwamba hii haikuwa launch ya vifaa pekee.

Kulikuwa na:

  • Vifaa vipya
  • Gemini Intelligence
  • AI features
  • Pixel 11 family
  • Pixel Watch 5
  • Pixel Tag
  • Pixel Buds
  • Health features
  • Partnerships
  • Na performance ya muziki mwishoni.

Lakini Gemini ndiyo iliyokuwa kama moyo wa show nzima.


🤯 Google Inasema Gemini Tayari Inatumiwa na Zaidi ya Watu Bilioni 1

Rick Osterloh alipoingia kwenye stage, Google ilianza kuzungumzia mabadiliko ambayo AI inaleta kwenye simu.

Google ilisema Gemini sasa inatumiwa na zaidi ya watu bilioni moja duniani, na kwenye Pixel 11 na Pixel Watch 5 wameleta mfumo wanaouita Gemini Intelligence hili niliongelea kabla HAPA.

Na hapa ndipo story inaanza kuwa tofauti.

Kwa sababu Google haikutaka tu kusema:

“Gemini ni smart.”

Wakaonyesha.


🧠 Gemini Intelligence: AI Inayoweza Kukusaidia Kufanya Kitu, Sio Kujibu Tu

Fikiria mtu amekutumia ujumbe akitaka kujua kama unaweza kukutana naye.

Badala ya wewe:

fungua Calendar → angalia ratiba → rudi kwenye message → andika jibu...

Google ilionyesha Gemini ikiwa na uwezo wa kusaidia kupitia mchakato huo.

Kwa ruhusa yako, Gemini inaweza kuangalia taarifa muhimu kwenye messages na calendar, kuelewa kama una nafasi, kisha kukusaidia kuandaa jibu.

Na jambo la kuvutia zaidi?

Jibu hilo unaweza kulishughulikia hata kupitia Pixel Watch 5.

Hii ndiyo tofauti kati ya:

AI inayokujibu

na

AI inayokusaidia kufanya kazi.


⌚ Na Huhitaji Kutoa Simu Mfukoni Kila Mara

Google pia ilionyesha namna Gemini Intelligence inavyounganisha experience ya simu na Pixel Watch 5.

Katika demonstration, mtumiaji aliweza kushughulikia baadhi ya mambo kupitia saa kwa kutumia hata pinch gesture (unaminya tu vidole) imekaa kama movie ya Sci-Fi ama?.

Kwa hiyo smartphone yako haiko peke yake tena.

Simu + Watch + Gemini = ecosystem moja.


📅 Gemini Inaweza Kukusaidia Kupanga Maisha Yako

Google pia ilionyesha Gemini ikisaidia kutafuta sehemu za kwenda na vitu vya kufanya.

Mfano mwingine ulioonyeshwa ulihusisha kutafuta sehemu za kucheza cricket na kupata chakula cha Kihindi huko Paris.

Na katika demonstration nyingine, Google ilionyesha matumizi ya Google Maps/OpenTable kwa amri ya sauti kusaidia kuweka au kuagiza meza kwenye restaurant.

Kwa lugha rahisi:

Unaanza kuzungumza na simu kama assistant halisi badala ya kuipa commands ndogo ndogo tu.


😳 Gemini Ilifanya Kitu Trevor Noah Alipozungumza

Hii ilikuwa moja ya demonstrations nilizozipenda zaidi.

Trevor Noah alizungumza kwa sauti, lakini kama binadamu wa kawaida:

“Umm…”

“Err…”

akasita...

akabadilisha mawazo...

Kisha akaanza tena.

Lakini hakulazimika kumwambia Gemini:

“Delete what I just said.”

Gemini iliweza kuelewa dhamira ya kile alichokuwa akijaribu kusema, badala ya kuandika kila neno lililotoka mdomoni kama lilivyo.

Na hiyo ni tofauti kubwa sana.

Google ilionyesha Voice Typing ikiwa imeboreshwa kuelewa mazungumzo ya kawaida, pamoja na kusita na kujisahihisha wakati mtu anaongea.

🤯 Hii ndiyo sehemu ya kushangaza:

AI inaanza kujaribu kuelewa “unamaanisha nini?” badala ya “umesema nini?”

Na hiyo inaweza kubadilisha kabisa namna tunavyoandika kwa kutumia voice.


🤯 CAMERA YA PIXEL ILIINGIA KWENYE LUGHA YA ALAMA

Hii ilikuwa moja ya moments ambazo zilifanya event iwe tofauti.

Google ilionyesha Sign to Text, ambapo camera inaweza kutambua American Sign Language (ASL) na kusaidia kuibadilisha kuwa maandishi.

Kwa hiyo camera ya simu haionekani tena kama:

“kifaa cha kupiga picha tu.”

Inaweza kuwa sehemu ya namna mtu anavyowasiliana.

Na hii ndiyo aina ya AI ambayo ukiona ikifanya kazi live, unaanza kuelewa kwa nini Google inawekeza sana kwenye Gemini.


📸 Na Camera? Google Ilikuwa Inaongea, Lakini Pia IKAONYESHA

Kuna tofauti kati ya kampuni kusema:

“Camera yetu ni nzuri.”

na kampuni kutumia camera hiyo kwenye tukio lenyewe.

Google ilionyesha uwezo wa camera mpya ikiwa na hadi 120x Zoom, pamoja na Instant Night Sight yenye kasi iliyoboreshwa kwa picha za usiku.

Lakini moja ya moments nilizozipenda zaidi ilikuja mwisho kabisa.


😳 WAIT... PERFORMANCE YA MWISHO ILIREKODIWA KWA PIXEL 11 PRO!

Event ilipofika mwisho, Trevor Noah alitangaza kwamba performance ya mwisho ilikuwa inarekodiwa kwa kutumia camera ya Pixel 11 Pro.

Kisha akaingia PinkPantheress na kufanya performance iliyofunga Made by Google 2026.

Hii ilikuwa njia nzuri sana ya Google kusema:

“Hatutaki kukuambia camera yetu inaweza kufanya nini. Tazama.”

🔥

Hii ndiyo sababu nilisema mwanzoni:

Camera haikuwa kelele za specs pekee. Google iliifanya sehemu ya show yenyewe na ilikua nzuri kinoma.


🎥 Magic Capture: Google Inataka Usikose Moment

Google pia ilionyesha Magic Capture.

Kipengele hiki kinaweza kunasa video na picha kwa wakati mmoja na kuchagua picha bora kutoka kwenye frames nyingi ili kusaidia kupata moment nzuri bila mtu kukosa pozi au kufumba macho.

Fikiria umechukua picha ya group:

Mmoja amefumba macho.

Mwingine anaangalia pembeni.

Mwingine bado anacheka.

Badala ya kuishia na picha mbaya, mfumo unajaribu kupata moment bora zaidi.

Hiyo ni AI inayotumika kwenye camera kwa namna ambayo mtu wa kawaida anaweza kuona faida yake.


✨ Highlight: Simu Inakujulisha Bila Kuichukua

Google pia ilionyesha Highlight.

Simu ikiwa imewekwa chini face down, mwanga wa rangi nyuma ya simu unaweza kukujulisha kuhusu simu au ujumbe unaoingia bila wewe kulazimika kugeuza simu.

Google hata ilifanya demonstration ya live na DJ Peggy Gou, ambapo Pixel ilionyesha mwanga wa teal.

Small feature.

Lakini ni moja ya zile features ambazo baada ya kuzizoea unaweza kujiuliza:

“Nilikuwa naishije bila hii?”


⚡ Tensor G6 Nayo Imeingia Mjengoni

Google pia ilionyesha processor mpya ya Tensor G6.

Hii ndiyo engine inayobeba sehemu kubwa ya mambo haya ya AI kwenye Pixel 11.

Na Google haikuacha kwenye performance pekee.

Kulikuwa na mazungumzo kuhusu:

  • Camera
  • AI
  • Battery
  • Security
  • Privacy
  • Miaka ya updates.

1. Ukichaji kwa Dakika 15:

  • Simu (Pixel 11 Pro): Ukiiweka kwenye chaji kwa dakika 15, inakupa matumizi ya hadi masaa 15 ya betri.

  • Saa (Pixel Watch 5): Ukiiweka kwenye chaji kwa dakika 15, inakupa matumizi ya karibu siku nzima (takriban masaa 24).

2. Ikijaa Kamili (100%):

  • Simu (Pixel 11 Pro): Ikijaa vizuri inatoa hadi masaa 30 ya matumizi endelevu kabla ya kuisha tena.

  • Saa (Pixel Watch 5):  Ikijaa vizuri inatumika hadi siku 4. 


🔐 Security Nayo Haikusahaulika

Google ilisisitiza pia upande wa privacy na security.

Mfumo unalenga kusaidia kupunguza spam na scams, huku Pixel ikiendelea kupata miaka 7 ya security updates.

Hii ni muhimu kwa sababu simu yenye AI yenye uwezo mkubwa inahitaji pia kuwa na mfumo wa usalama unaoaminika.


⌚ Pixel Watch 5 Haikuja Kwa Mapambo

Google haikuiweka Pixel Watch 5 pembeni.

Kulikuwa na Health Guardian, Google Health Coach na vipengele vingine vya afya vilivyoonyeshwa kwenye event.

Google ilionyesha uwezo wa kufuatilia baadhi ya trends za afya, pamoja na vipengele vya kugundua hali za dharura na kusaidia kwenye mazoezi.

Pia ilionyesha ushirikiano wa kamba za Pixel Watch na Steph Curry.

Na Google ikatambulisha pia Pixel Tag, kifaa kidogo cha kusaidia kufuatilia vitu kama funguo, wallet au begi unakishikisha katika vitu vyako kitu kikipotea una-track location.


🎧 Na Pixel Buds Pro 2 Zimepata Maboresho

Google pia ilizungumzia Pixel Buds Pro 2, ikiwa na maboresho yanayohusiana na noise cancellation wakati wa mazoezi na interaction yake na Pixel Watch.

Hii inaonyesha kitu kimoja:

Google haitaki Pixel iwe simu pekee.

Wanajenga ecosystem.


🍎 Unataka Kuhama iPhone kwenda Pixel? Google Imekuja na Jibu

Hapa Google iligusa moja ya maeneo ambayo Pixel imekuwa ikihitaji kushughulikia:

switching.

Katika event, Google ilionyesha namna ya kuhama kutoka iPhone/iOS kwenda Pixel, ikiwemo kuhamisha:

  • Picha
  • Video
  • Messages
  • eSIM
  • Wi-Fi
  • Passwords

na pia ikatangaza Quick Share inayoweza kufanya kazi na MacBooks na iPhones.

Kwa mtu ambaye amekuwa kwenye Apple ecosystem kwa miaka mingi, hii inaweza kuwa muhimu sana.


⚽🔥 HALAFU GOOGLE IKASEMA: “TEAM PIXEL”

Sasa hapa ndipo event ilipata flavor nyingine.

Trevor Noah alipokea surprise kutoka kwa Steven Gerrard, kisha Google ikatangaza ushirikiano wa Team Pixel na baadhi ya majina makubwa kabisa kwenye soka.

Majina yaliyotangazwa yalikuwa:

Liverpool FC
Arsenal
Paris Saint-Germain (PSG)
FC Bayern
FC Barcelona

Pamoja na ushirikiano unaohusisha WNBA na F1 McLaren.

Kwa hiyo sasa Google haijengi tu:

Pixel phone.

Inaonekana pia inajenga:

TEAM PIXEL.

Na kwa brand, hiyo ni move kubwa.


🏙️ Google Pia Imefungua Duka Jipya Tokyo

Katikati ya event, Google ilionyesha pia habari kuhusu Google Store mpya huko Omotesando, Tokyo, Japan, ikiwa sehemu ya kuendeleza experience yake ya hardware kwa watumiaji.


🥵 Na Hatujaishia Hapo...

Kuna jambo moja ambalo linanifanya niione Made by Google 2026 tofauti.

Google ilionyesha:

Phone.

Watch.

Buds.

Tag.

Gemini.

AI.

Health.

Camera.

Translation.

Accessibility.

Sports partnerships.

Na hata smart eyewear ipo kwenye direction yao.

Hii si tena kampuni inayotaka kukuuzia smartphone moja.

Google inajaribu kujenga dunia ambayo vifaa vyake vinaelewana na AI yake inakusaidia kuviongoza.


🤯 Kitu Kikubwa Nilichokiona Leo

Kama kuna kitu kimoja ningebaki nacho baada ya kuangalia event hii yote, ni hiki:

Google imeanza kuifanya AI ionekane kama sehemu ya maisha ya kawaida.

Sio:

“Fungua Gemini.”

“Andika prompt.”

“Subiri jibu.”

Bali:

“Nina message.”

“Angalia kama niko free.”

“Nisaidie kujibu.”

“Ninazungumza.”

“Nimejirekebisha.”

“Elewa nilichomaanisha.”

“Ninazungumza lugha nyingine.”

“Mtu anatumia sign language.”

“Nataka kupiga picha.”

“Nataka kujua kilichopo mbele yangu.”

Na hapo ndipo Gemini Intelligence inaanza kuwa interesting kweli.


🚨 NA HII NDIYO STORY YA LEO KWA 246 ONLINE

Kama ulikuwa umelala wakati sisi tuko macho tukisubiri event ianze 😅, umechelewa kidogo lakini hujapitwa.

Kwa sababu hii ndiyo ilikuwa Made by Google 2026.

Na bado hatujaingia kwa undani kwenye Pixel 11 yenyewe.

Hatujaanza kuchambua:

📱 Pixel 11
📱 Pixel 11 Pro
📱 Pixel 11 Pro XL
📱 Pixel 11 Pro Fold
⌚ Pixel Watch 5
🎧 Pixel Buds
📍 Pixel Tag
🧠 Gemini Intelligence
📸 Camera
⚡ Tensor G6
🔐 Security
🔋 Battery
✨ Magic Capture
na mambo mengine yaliyotangazwa.

Hizo tunazifungua moja baada ya nyingine hapa 246 ONLINE.


❤️ Kama Umeona Hii Ni Kali, USIACHE MWINGINE APITWE

Kuna mtu wako WhatsApp au Facebook ambaye alikuwa amelala wakati sisi tuko macho saa 1:00 usiku tukisubiri Google ianze. 😂

Mtumie hii article.

Kwa sababu leo Google haikutoa tu simu mpya.

Google imetupa picha ya namna inavyoiona future ya simu + AI.

Na kama ulifikiri hapo ndiyo tumemaliza...

Hapana.

🔥 Hii ilikuwa trailer.

Sasa tunaanza kuifungua Pixel 11 yenyewe.


Imeandaliwa na 246 ONLINE.

246
246 Admin
Mwandishi · 246 ONLINE
Anaandika kuhusu AI, PC na usalama wa kidigitali kwa lugha ya Kiswahili, ili teknolojia ieleweke kwa urahisi kwa Watanzania na Waswahili duniani kote.
Jiunge na 246 ONLINE
Pata makala mpya moja kwa moja
Maoni
0
Anonymous inaruhusiwa — hakuna lazima ya akaunti.