Karibuni tena Mjengoni, 246 Online! πΉπΏ
Vipi wakuu? Kama ulipitia Part 1 na Part 2, sasa hivi utakuwa unatembea kifua mbele ofisini au chuoni. Ile spidi ya kutumia Ctrl + Backspace na Virtual Desktops inawafanya watu wakuone kama mchawi wa kompyuta, sindio? π
Leo tunahitimisha huu mchezo. Kwenye Part 3, hatufanyi mchezo wa watoto. Tunaingia kwenye uvungu wa Windows. Hapa tunagusa Advanced System Commands, tunaingia kwenye CMD (ule ukurasa mweusi wa "Hackers"), na tunacheki maujanja mapya ya Windows 11 ambayo watu wengi hawayajui.
Onyo: Hizi shortcuts zina nguvu. Ukizijua, usiringe sana! π
Twende kazi! π
SEHEMU YA 11: System & Admin Commands (Utawala wa PC)
Hizi ni shortcuts za haraka za kufungua settings ambazo mara nyingi zimefichwa mbali.
Win + I: Settings App (Acha kuzunguka kutafuta settings kwenye Start Menu. Piga hii uingie moja kwa moja kurekebisha WiFi, Display, n.k).
Win + X: Quick Link Menu (Hii ni menyu ya siri! Inafunguka kushoto chini. Hapo utapata Device Manager, Disk Management, na PowerShell haraka sana).
Win + L: Lock PC (Unataka kwenda washroom au kuchukua maji? Piga hii kufunga PC fasta ili "Wambea" wasichungulie kazi zako).
Win + R: Run Command (Kiboksi cha maajabu. Ukikifungua hichi, unaweza kuandika cmd, calc (calculator), au temp kusafisha uchafu).
Win + Pause/Break: System Properties (Unataka kujua PC yako ina RAM ngapi na Processor gani? Piga hii shortcut upate majibu papo hapo).
Ctrl + Shift + Esc: Task Manager (PC imeganda? Program imekataa kutoka? Usizime kwa button! Piga hii, tafuta hiyo program, bonyeza "End Task". Mchezo umeisha).
SEHEMU YA 12: CMD & Run Commands ("Hacker" Vibes) π΅️♂️
Hizi zinatumika ndani ya kile kiboksi cha Win + R au kwenye Command Prompt (CMD). Ukitumia hizi mbele ya watu, watajua wewe ni IT expert.
cmd: (Andika kwenye Run) Kufungua Command Prompt.
calc: (Andika kwenye Run) Kufungua Calculator chap!
mspaint: (Andika kwenye Run) Kufungua Paint kuchora au kuedit picha haraka.
notepad: (Andika kwenye Run) Kufungua Notepad kuandika vitu haraka.
osk: On-Screen Keyboard (Keyboard yako ya kawaida imekufa baadhi ya button? Piga hii uletewe keyboard ya kiooni utumie mouse).
dxdiag: (Andika kwenye Run) Hii inakupa siri zote za Display na Sound ya PC yako. Muhimu sana ukiwa unanunua PC kwa mtu, piga hii ukague specs zake.
SEHEMU YA 13: Windows 11 Specials (Vitu Vipya!) ✨
Kama unatumia Windows 11, Microsoft wameongeza shortcuts tamu sana za kurahisisha maisha na kuifanya PC ionekane ya kisasa.
Win + A: Quick Settings (Fungua WiFi, Bluetooth, Brightness, na Volume haraka upande wa kulia).
Win + N: Notification Center & Calendar (Cheki tarehe na meseji zako zote hapa).
Win + W: Widgets (Fungua habari, hali ya hewa, na matokeo ya mpira upande wa kushoto).
Win + Z: Snap Layouts (Hii ni KIBOKO! Unataka kupanga windows 4 kwenye screen moja? Piga hii uchague mpangilio/layout unayotaka, Windows itakupangia yenyewe).
Win + K: Cast (Unataka kuunganisha PC na TV bila waya? Piga hii utafute TV yako).
Win + H: Voice Typing (Umechoka kuandika? Piga hii, ongea, na PC itakuandikia. Note: Inafanya kazi vizuri kwa Kiingereza).
SEHEMU YA 14: Clipboard History (Rudia Tulichojifunza) ♻️
Hii tuliigusia kwenye video zetu za YouTube (@246_Online), lakini lazima tuiweke hapa kwa maandishi maana ni muhimu sana.
Win + V: Clipboard History (Acha kutumia Ctrl+V pekee! Ukicopy vitu vitatu tofauti, Ctrl+V inakupa cha mwisho tu. Win+V inakupa list ya vitu vyote ulivyocopy kuanzia asubuhi. Washa hii leo, itakuokoa sana!)
HITIMISHO: Umemaliza Kozi! π
Hongera Mwanangu! ππ
Kama umefuatilia Part 1, 2 na 3, wewe sasa sio mtumiaji wa kawaida wa Kompyuta. Wewe ni Power User. Idadi ya Shortcuts ulizonazo kichwani zinatosha kuendesha ofisi nzima bila kugusa mouse.
Zoezi la Mwisho: Wiki hii, jaribu kutumia Win + V (Clipboard History) na Win + L (Lock PC) kila siku. Hizi mbili zitabadilisha maisha yako ya kazi.
Kama bado hujacheki video zetu za jinsi ya kutumia hizi shortcuts kwa vitendo, nenda YouTube sasa hivi:
πΊ YouTube:
Kumbuka: Ujanja ni Ku-Share! Mtumie link ya post hii mshikaji wako anayeteseka na mouse, msaidie aokoe muda.
Imeandaliwa na: Admin, 246 Online. (Tunakupa maujanja, wewe kazi yako ni kutoboa!) π
Maoni