246 ONLINE

🚨 APPLE YABADILI MPANGO! iPHONE 18 YA KAWAIDA INAWEZA KUCHELEWA HADI 2027 😳

246
246 Admin
Mwandishi — 246 ONLINE
Agosti 16, 2026
🚨 APPLE YABADILI MPANGO! iPHONE 18 YA KAWAIDA INAWEZA KUCHELEWA HADI 2027 😳

September bila iPhone 18 ya kawaida? Apple anaweza kufanya hivyo! 😳

Kuna kitu kinaweza kubadilika kwenye ratiba ambayo Apple ametuzoesha kwa miaka mingi.

Kwa kawaida tunajua:

September → iPhone mpya → Pro + iPhone ya kawaida.

Lakini ripoti mpya zinaonyesha kwamba iPhone 18 ya kawaida inaweza isije pamoja na Pro models mwaka 2026.

Badala yake, inaweza kusubiri hadi 2027.

😳 Subiri... iPhone 18 itaahirishwa?

Apple iPhone 18 inaweza kucheleweshwa hadi 2027 huku foldable iPhone ikitarajiwa 2026: 246 Online


📱 Sasa 2026 tunaweza kuona iPhone gani?

Kulingana na taarifa hiyo, Apple inaweza kuweka nguvu zaidi kwenye upande wa premium mwaka 2026, ukiwemo:

  • iPhone 18 Pro
  • iPhone 18 Pro Max
  • 🤯 iPhone foldable, inayotarajiwa kuwa moja ya bidhaa kubwa zaidi za Apple

Wakati huo, iPhone 18 ya kawaida inaweza kuja baadaye.

Hii inaweza kumaanisha Apple inaanza kugawa uzinduzi wa iPhone katika vipindi viwili badala ya kutupa lineup yote kwa wakati mmoja.


🤔 Kwa nini Apple afanye hivi?

Moja ya sababu zinazotajwa ni changamoto kwenye upatikanaji wa memory/chips, jambo ambalo linaweza kuifanya Apple kuelekeza resources zaidi kwenye simu zake za bei ya juu.

Lakini kuna jambo jingine la kuvutia.

Apple anaweza kutaka 2026 iwe mwaka wa iPhone za “premium”.

Badala ya attention kugawanyika kati ya iPhone ya kawaida na Pro, spotlight inaweza kwenda kwenye:

iPhone 18 Pro + Pro Max + foldable iPhone. 🔥


🤯 Na Hii Inaweza Kubadilisha September Event

Fikiria Apple anaingia stage mwaka 2026 bila kutangaza iPhone 18 ya kawaida.

Badala yake...

“This is our new iPhone Pro.”

Halafu:

“And one more thing...” 👀

FOLDABLE iPHONE.

Foldable iPhone - 246 Online blog
Hapo Apple event inaweza kuwa moja ya launches zinazozungumziwa zaidi mwaka huo.

Lakini kumbuka: Apple bado hajathibitisha rasmi ratiba hii. Hii ni taarifa inayotokana na ripoti, hivyo tunapaswa kuichukulia kama reported plan, si tangazo rasmi.


🔥 Kwa 246 ONLINE

Kama mpango huu utatimia, 2026 inaweza kuwa mwaka ambao Apple anabadilisha kabisa namna iPhone inavyotoka.

Na swali sasa ni moja:

Je, Apple atatutoa kwenye iPhone ya kawaida... na kutupeleka kwenye foldable? 👀
TULIONGELEA iPhone ya kukunja hapa kama hujaijua hii bonyeza hapa.

Tutafuatilia.

246
246 Admin
Mwandishi · 246 ONLINE
Anaandika kuhusu AI, PC na usalama wa kidigitali kwa lugha ya Kiswahili, ili teknolojia ieleweke kwa urahisi kwa Watanzania na Waswahili duniani kote.
Jiunge na 246 ONLINE
Pata makala mpya moja kwa moja
Maoni
0
Anonymous inaruhusiwa — hakuna lazima ya akaunti.