246
ONLINE
INITIALIZING
LIVE
Inapakia makala... 246 ONLINE — Intelligence and Information First
KIOO CHA LAPTOP NI KIDOGO? Jinsi ya Kugeuza Simu au Tablet Yako Kuwa "Monitor ya Pili" (Second Screen) ya Kompyuta Yako BURE (Wireless Extension)
Simon Guyashi
Simon Guyashi
Mwandishi — 246 ONLINE
May 08, 2026
⏱ ...

KIOO CHA LAPTOP NI KIDOGO? Jinsi ya Kugeuza Simu au Tablet Yako Kuwa "Monitor ya Pili" (Second Screen) ya Kompyuta Yako BURE (Wireless Extension)

 Habari Mkuu wa 246 Online!

Kuna wakati unafanya kazi kwenye Kompyuta, madirisha (Windows) yamejaa. Unataka kuandika ripoti huku unasoma data sehemu nyingine, inabidi kila saa ufunue na kufunga tabs (Alt+Tab). Inachosha na inapunguza kasi ya kazi.

Watu wa majuu hununua "Monitor" za ziada za laki 3 au 4 ili kuongeza uwanja wa kazi (Dual Monitor Setup).

Lakini wewe mjanja wa 246 Online, unayo Monitor mfukoni mwako!

Leo tunakufundisha jinsi ya kutumia simu yako ya Android (au Tablet ya zamani iliyolala ndani) kuifanya iwe kioo cha nyongeza cha Kompyuta yako. Utaweza kuhamisha mouse na programu kutoka kwenye Laptop kwenda kwenye Simu kwa njia ya Wi-Fi.

Geuza ofisi yako iwe ya kisasa sasa hivi... πŸ’»➕πŸ“±



MAHITAJI

  1. Kompyuta (Windows 10 au 11).
  2. Simu au Tablet (Android au iOS).
  3. Zote ziwe zimeunganishwa kwenye Wi-Fi moja (Au washa Hotspot ya simu uunganishe PC, hata kama huna bando).

HATUA YA 1: Pakua "Spacedesk" Kwenye Kompyuta

Hii ni software nyepesi na ya bure kabisa.

  1. Kwenye Kompyuta yako, ingia Google na utafute "Spacedesk Driver".
  2. Ingia kwenye website yao rasmi (spacedesk.net).
  3. Pakua toleo la Windows (32-bit au 64-bit kulingana na PC yako).
  4. Install hiyo driver kwenye kompyuta (Next > Next > Install).

HATUA YA 2: Pakua "Spacedesk" Kwenye Simu 

  1. Chukua simu au Tablet yako.
  2. Ingia Play Store (au App Store).
  3. Tafuta na upakue App inaitwa "Spacedesk".

HATUA YA 3: Unganisha (Connect) πŸ”—

Hapa ndipo unipoona maajabu.

  1. Hakikisha Driver ina-run kwenye Kompyuta (Utaona icon yake kule chini kulia karibu na saa).
  2. Fungua App ya Spacedesk kwenye simu.
  3. Moja kwa moja itaiona Kompyuta yako (itaandika Jina la PC na IP Address).
  4. Bonyeza jina la Kompyuta hiyo kwenye simu.

PAPO HAPO: Kioo cha simu yako kitabadilika na kuwa Desktop ya Windows! Utaona Background ya kompyuta yako imetokea kwenye simu.


HATUA YA 4: Jinsi ya Kutumia (Extension Mode)

Kwa sasa inaweza kuwa inaonyesha kitu kile kile (Duplicate). Sisi tunataka iwe "Extension" (Eneo la ziada).

  1. Kwenye Kompyuta, Right-click sehemu tupu kwenye Desktop.
  2. Chagua Display Settings.
  3. Utaona vioo viwili (1 na 2).
  4. Shuka chini kwenye Multiple displays na uchague "Extend these displays".
  5. Bonyeza Apply.

Sasa jaribu kupeleka Mouse yako upande wa kulia au kushoto mwa screen ya laptop... ITAINGIA NDANI YA SIMU! πŸ–±️

Sasa unaweza:

  • Kufungua YouTube ukaiburuta (Drag) iende ikae kwenye simu.
  • Kuweka Tools za Photoshop kwenye simu huku unapigia kazi kwenye Laptop.
  • Kuweka Chat za WhatsApp kwenye simu huku unafanya kazi kwenye PC.

VIPENGELE VYA ZIADA (Touchscreen)

Uzuri wa njia hii ni kwamba Touchscreen ya simu inafanya kazi kwenye Windows!

  • Unaweza kubonyeza vitu kwenye Windows kwa kutumia kidole chako kwenye simu. Ni kama umenunua Laptop yenye Touchscreen kwa gharama ya bure!


HITIMISHO

Hii ni "Setup" ya kibabe sana kwa watu wabunifu (Creators), Traders (wa Forex), na Wanafunzi. Tablet yako ya zamani isikae tu kabatini, igeuze kuwa Monitor.

Jaribu hii setup, piga picha ofisi yako ikiwa na vioo viwili, post status uone heshima itakavyorudi!

USIPITWE: [Kompyuta Haina Fingerprint? Jinsi ya kutumia Fingerprint ya Simu yako kufungua (Unlock) Laptop yako kwa mbali! (Remote Fingerprint Unlock)]

Soma Pia Hizi
Maoni
0
Anonymous inaruhusiwa — hakuna lazima ya akaunti.
246