Google Antigravity 2.0: Mapinduzi ya AI Yanayotengeneza Mfumo wa Uendeshaji (OS) Kutoka Sifuri!
Mambo vipi mdau wa 246 Online! Kama ulikuwa unafikiri AI inaishia tu kuandika barua pepe, insha, au kukurekebishia makosa ya kisarufi, basi Google wameamua kuwasha moto mwingine mkali kwenye mkutano wao wa Google I/O 2026.
Google wametambulisha rasmi Google Antigravity 2.0 —App ya kompyuta (Desktop) ambayo sasa hivi haiji tu kama "kifaa cha AI", bali kama Mhandisi Kamili wa Programu (Agent-First Development Platform)
Kama unataka kujua ni kwa namna gani teknolojia hii inaenda kubadilisha maisha ya ma-developer na wapenzi wa tech, twende sawa!
Antigravity 2.0 Ni Nini Hasa?
Hapo awali (mwezi Novemba), Antigravity ilizinduliwa kama IDE (kifaa cha kuandikia code) kilichosaidiwa na AI. Lakini toleo hili jipya la 2.0 limekuja kivingine kabisa. Ni mfumo unaojitegemea (Standalone Desktop Application) unaoongozwa na mawakala wa AI (Agents) wanaoweza kufanya kazi kwa kushirikiana (Multi-agent orchestration) kukamilisha kazi kubwa za coding bila mwanadamu kushika kibodi kila saa ..
Kitu kinachosimamisha nywele ni kwamba, Mkurugenzi Mtendaji wa Google, Sundar Pichai, mwenyewe alitumia mfumo huu hivi karibuni kurekebisha makosa (bugs) kwenye mifumo ya Google!.
Mtihani Mzito: AI Inatengeneza Operating System Ndani ya Masaa 12!
Ili kuonyesha uwezo wa mwisho wa chombo hiki, wahandisi wa Google walikipa kazi moja ngumu zaidi kwenye ulimwengu wa kompyuta: Kutengeneza Mfumo mzima wa Uendeshaji (Operating System) kutoka sifuri (Scratch). .
Kazi kama hii huchukua miezi mingi kwa timu za wanadamu, lakini Antigravity 2.0 ikishirikiana na modeli mpya ya Gemini 3.5 Flash ilifanya maajabu haya:
Mawakala (Sub-agents) 93 walifanya kazi kwa pamoja kwa njia ya mtandao.
Walituma requests zaidi ya 15,000 kwenye modeli ya AI.
Walichakata jumla ya tokens bilioni 2.6 ].
Masaa 12 tu yalosha! Mradi ulikuwa mtupu, lakini ndani ya masaa hayo kulikuwa na OS inayofanya kazi, kuanzia bootloader, mifumo ya kumbukumbu (memory management), hadi file system.
Na sehemu nzuri zaidi? Gharama ya API kutengeneza OS hiyo yote haikuzidi Dola $1,000 za Kimarekani shukrani kwa unafuu wa Gemini 3.5 Flash!
Je, OS Hiyo Inafanya Kazi Kweli? (Hadi Game la DOOM Limechezeka!)
Kwenye demo ya Live iliyoonyeshwa kwenye video ya sl (typo ya ls) na treni ikapita kwenye kioo ikiwa na logo ya Antigravity.
Lakini je, OS imekamilika bila game la DOOM? Mwanzoni game halikuwaka kwa sababu OS ilikuwa haina video and keyboard drivers. Mwasilishaji alichofanya ni kuandika ombi tu (Prompt) ndani ya Antigravity 2.0 akiiambia AI itengeneze driver hizo. Ndani ya dakika chache, AI iliandika code, ikazifanyia majaribio, na game la DOOM likawaka na kuchezeka vizuri kabisa!.
Sifa Nyingine za Kipekee za Antigravity 2.0:
Ina Kasi ya Ajabu (12x Faster): Modeli ya Gemini 3.5 Flash imeboreshwa ndani ya Antigravity na kuwa na kasi mara 12 zaidi kuliko kawaida ili kuendana na uhitaji mkubwa wa tokens wakati wa kuandika code.
Cli Experience & SDK: Sasa inakuja na CLI kamili na SDK yake kwa ajili ya ma-developer wanaopenda kufanyia kazi kwenye terminal.
Sauti ya Native (Voice Support): Unaweza kuongea nayo na ikakuelewa kwa kutumia nguvu ya Gemini Audio Models.
Ujumuishaji (Integrations): Imeunganishwa moja kwa moja na mifumo kama Android, Firebase, na Google AI Studio.
Neno la Mwisho kutoka 246 TECHHUB
Huu ni uthibitisho wa wazi kuwa ulimwengu wa uundaji wa programu (software development) unabadilika kwa kasi ya mwanga. Miradi ya kihandisi inayochukua siku nyingi sasa inaisha ndani ya masaa au dakika chache tu.
Kama unataka kujionea mwenyewe au kuanza kuitumia, Google wameifanya Antigravity 2.0 kupatikana kimataifa kwa kila mtu kuanzia leo! Tembelea tovuti yao rasmi hapa:
Je, unaona AI itachukua nafasi za ma-programmer kabisa au itatusaidia kuwa wabunifu zaidi? Dondosha maoni yako hapo chini!
CHECK HII MAAJABU YA CLAUDE AI
