Wanangu wa 246 ONLINE, leo hatuibi Status wala View Once. Leo tunamvulia kofia (ya ufundi!) mwamba mmoja anayeitwa Jean-Baptiste Kempf. Kama unatumia kompyuta au simu, basi asilimia 99 unajua lile koni la rangi ya machungwa la VLC Media Player.
Lakini unajua siri iliyopo nyuma ya hilo koni? Mwamba alikataa ofa ya mamilioni ya dola (zaidi ya Shilingi Bilioni 100 za Kitanzania!) ili wewe uendelee kuangalia muvi na kusikiliza ngoma bure bila matangazo ya hovyo.
π ️ Kwanini VLC ni "King" wa Media Players?
Wakati makampuni mengine kama Microsoft na Apple yakikuzingua na "Codecs" (lazima ununue au u-download vikorokoro ili video icheze), VLC inakula kila kitu. Iwe ni MP4, MKV, AVI, au hata ma-file yaliyoharibika—VLC hachagui chakula!
π° Ofa za "Kishetani" Alizozikataa
Jean-Baptiste Kempf amewahi kuwekewa mezani ofa za hatari:
- Matangazo (Ads): Kampuni za matangazo zilimtaka aweke "Banner ads" ndani ya VLC. Alikataa.
- Data Mining: Walimtaka auze data za watumiaji (unachoangalia, unapoangalia). Alikataa.
- Kuiuza Kampuni: Matajiri walitaka kuinunua VideoLAN. Aligoma.
Kwanini? Alisema: "Nina furaha na maisha yangu, na sitaki kuharibu kitu ambacho kinawasaidia mamilioni ya watu duniani kwa ajili ya pesa ambazo hata sitazitumia zote." Huu ndio unyama ambao Mark Zuckerberg hawezi kuufanya!
π Vitu Ambavyo Hujui Kuhusu VLC (Maujanja ya Ndani):
Kwenye blog yetu tunapenda maujanja, basi fahamu hili:
- VLC ni Video Converter: Unaweza kubadili video kwenda MP3 au format nyingine ukitumia VLC pekee.
- Kurekodi Screen: VLC inaweza kurekodi screen ya PC yako bila kuhitaji App nyingine.
- Inacheza YouTube: Unaweza kuweka link ya YouTube ndani ya VLC na ukaangalia video bila matangazo ya YouTube kukusumbua!
Maoni