246
ONLINE
INITIALIZING
LIVE
Inapakia makala... 246 ONLINE — Intelligence and Information First
Usiwe Chawa wa Wi-Fi: Jinsi ya Kuiona (View) Password ya Wi-Fi Yoyote Iliyoconnect Kwenye Simu Yako Bila Root! πŸ“ΆπŸ”“πŸ‘οΈ
Simon Guyashi
Simon Guyashi
Mwandishi — 246 ONLINE
January 26, 2026
⏱ ...

Usiwe Chawa wa Wi-Fi: Jinsi ya Kuiona (View) Password ya Wi-Fi Yoyote Iliyoconnect Kwenye Simu Yako Bila Root! πŸ“ΆπŸ”“πŸ‘️

 Wanangu wa 246 Online, Leo tunafanya "Sharing is Caring"! 🀝

Hii imetutokea wote. Umeenda sehemu (cafe, chuo, au kwa tajiri), wamekuunganishia Wi-Fi kwenye simu yako lakini wamekuficha password. Ghafla mshkaji wako anakuja, anataka umuunge. Unabaki kusema "Dah, sijui password mwanangu."

Acha unyonge. Leo nakupa maujanja ya Ku-Extract Password kutoka kwenye simu yako uione kwa macho (Text) ili umtajie mshkaji au uiandike kwenye Laptop yako.

Hii inafanya kazi kwenye Android 10, 11, 12, 13, na 14.



πŸ› ️ Hatua kwa Hatua (Dakika 1)

Step 1: Pata Mchoro (QR Code)

  1. Ingia Settings > Wi-Fi (au Connections).

  2. Bonyeza jina la hiyo Wi-Fi ambayo umeunganishwa nayo sasa hivi.

  3. Utaona kitufe kimeandikwa "Share" au icon ya QR Code. Bonyeza hapo.

  4. Piga Screenshot ya hiyo QR Code inayotokea. (Hapa ndipo password ilipofichwa).

Step 2: Ifumbue Password (Decode) Simu nyingi za kisasa (Samsung/Xiaomi) ukiangalia chini ya hiyo QR Code zinaandika password kwa maandishi madogo. Kama simu yako haijaandika, fanya hivi:

  1. Fungua App ya Google Photos au Google Lens (ipo kwenye kila simu ya Android).

  2. Fungua ile Screenshot uliyopiga.

  3. Bonyeza kitufe cha "Lens" (kile cha kutafuta).

  4. Boom! πŸ’₯ Google Lens itaisoma hiyo picha na chini kabisa itaandika:

    • Network Name: [Jina la Wi-Fi]

    • Password: [Hapa itaonesha Password Halisi]

πŸ’‘ Njia ya "Kihuni" Zaidi (Kama huna Google Lens)

Kama hutaki kutumia Google Lens, tumia browser yako:

  1. Ingia kwenye site hii: zxing.org (Hii ni site ya decoder).

  2. Upload ile screenshot yako.

  3. Bonyeza "Submit".

  4. Kwenye majibu, angalia mstari ulioandikwa "Raw Text". Password yako itaonekana hapo Live bila chenga!

⚠️ Matumizi (Disclaimer)

Hii trick ni kwa ajili ya ku-share internet na washkaji zako tu. Usitumie kudukua Wi-Fi za serikali au sehemu nyeti. 246 Online tunataka uwe mjanja, sio mhalifu! πŸ˜‰


Hitimisho: Sasa hivi ukifika sehemu wakaweka password, wewe ndio unakuwa "Admin". Unaweza kuwapa washkaji password hiyo hiyo.

Jaribu sasa hivi kwenye Wi-Fi uliyoconnect nayo, uone kama utaipata password yake!

MORE HACKS

#246Online #WiFiHack #PasswordReveal #AndroidTricks #FreeInternet

Soma Pia Hizi
Maoni
0
Anonymous inaruhusiwa — hakuna lazima ya akaunti.
246