246
ONLINE
INITIALIZING
LIVE
Inapakia makala... 246 ONLINE — Intelligence and Information First
Jinsi ya Kusoma Meseji za WhatsApp Zilizofutwa ("This message was deleted") Bila GBWhatsApp Wala Ku-Install App Yoyote! πŸ—‘οΈπŸ‘€βœ¨
Simon Guyashi
Simon Guyashi
Mwandishi — 246 ONLINE
March 16, 2026
⏱ ...

Jinsi ya Kusoma Meseji za WhatsApp Zilizofutwa ("This message was deleted") Bila GBWhatsApp Wala Ku-Install App Yoyote! πŸ—‘️πŸ‘€✨

 Wanangu wa 246 Online, Leo tunafufua waliokufa! πŸ’€

Unajua ile kero. Simu inalia Ting! Uko bafuni. Unatoka nduki kuangalia, unakuta imeandika:

  • "This message was deleted"
  • "This message was deleted"

Unamuuliza "Ulifuta nini?", anakujibu "Ah, nilikosea namba". Unajua anakudanganya lakini huna ushahidi.

Watu wengi wanakimbilia GBWhatsApp, lakini siku hizi WhatsApp wanapiga ban namba zinazotumia GB. Acha kuhangaika. Simu yako ya Android (Android 11 na kuendelea) ina Log Book ya siri ambayo inatunza kumbukumbu ya kila notification inayoingia, hata kama mwenye kutuma ameifuta!




πŸ› ️ Hatua kwa Hatua (Dakika 1 Tu)

Hii trick ipo kwenye Settings za simu yako, ila imefichwa.

  1. Nenda Settings.
  2. Ingia Notifications (au Apps & Notifications)
  3. Bonyeza "Notification History". (Kama huioni, bonyeza "Advanced Settings" kwanza).
  4. Kitufe hicho kitakuwa kimezimwa (Off). KIWASHE (Turn On) sasa hivi!

🎩 The Magic (Maajabu Yake)

Kuanzia sasa ukiwasha hiyo setting:

  1. Mtu akikutumia meseji WhatsApp: "Njoo nikupe hela yako."
  2. Ghafla akajishtukia na Kuifuta: "This message was deleted."
  3. Wewe usiwe na wasiwasi.
  4. Nenda Settings > Notifications > Notification History.
  5. Shuka chini kwenye list ya WhatsApp.
  6. BOOM! πŸ’₯ Utaona meseji yake halisi "Njoo nikupe hela yako" bado ipo hapo imehifadhiwa, ingawa kule WhatsApp imefutika!

πŸ’‘ Faida Zake

  • Usalama: Huna haja ya kuweka ma-app ya ajabu yanayoiba data zako.
  • Ushahindi: Unakuwa na ushahidi wa kila kitu.
  • Amani: Hakuna tena siri. Unajua kila kilichofutwa.

(Kumbuka: Hii inafanya kazi kwa meseji za maandishi (Text). Picha na Video zikifutwa haziwezi kurudi hapa, lakini maneno yanarudi yote!)


Hitimisho: Washa Notification History leo, uwe unacheka tu pindi watu wanapofuta meseji zao wakidhani wameficha ujinga. Wewe unayo nakala kule Settings.

Ukifanikiwa kuona meseji iliyofutwa, rudi hapa utupe ushuhuda!

#246Online #WhatsAppTricks #DeletedMessages #NotificationHistory #AndroidSecrets #HakunaSiri

Soma Pia Hizi
Maoni
0
Anonymous inaruhusiwa — hakuna lazima ya akaunti.
246