Karibuni tena wanangu wa 246 Online!
Vipi, ile Part 1 imewakaa? Mshazoea kutumia Ctrl + C na Ctrl + V mpaka mouse imeanza kupata vumbi? Safi sana.
Kama bado unasuasua na Part 1, [BONYEZA HAPA UKAISOME KWANZA]. Lakini kama wewe ni jembe na unataka kuongeza "swag" za kidijitali, basi uko mahali sahihi.
Leo kwenye Part 2, hatucheki na nyani. Tunaingia kwenye shortcuts ambazo waandishi, bloggers, na watu wa maofisini wanazitumia kufanya kazi ya masaa mawili ndani ya dakika 20.
Tunaenda kufungua lile sanduku la "Expansion Packs" tulizozitaja mwanzo. Vaa mkanda, chukua soda baridi... twende kazi!
SEHEMU YA 6: Text Editing Ninja (Uandishi wa Kasi ya 5G)
Hapa ndipo penye utamu. Acha tabia ya kufuta herufi moja moja kama kuku anadonyoa mahindi. Tumia hizi uwe professional.
Kucheza na Maneno (Navigation)
Ctrl + Left/Right Arrow: Ruka neno zima! (Badala ya kishale kwenda herufi moja moja
t-u-k-t-u-k, hii inarukagari-kwa-gari. Speed kali!).Ctrl + Up/Down Arrow: Ruka paragraph nzima (Panda juu au shuka chini kwa kasi).
Home: Nenda mwanzo kabisa wa mstari unaoandika (Fasta kama umeme).
End: Nenda mwisho wa mstari (Ukitaka kuongeza nukta mwisho wa sentensi bila kushika mouse).
Ctrl + Home: Nenda mwanzo kabisa wa Document (Hata kama ina page 100, utafika page 1 sekunde hiyohiyo).
Ctrl + End: Nenda mwisho kabisa wa Document (Unataka kuweka saini mwisho? Bonyeza hii).
Uchaguzi na Ufutaji (Selection & Deletion)
Shift + Left/Right Arrow: Chagua (Highlight) herufi moja moja.
Ctrl + Shift + Left/Right Arrow: HII NI MUHIMU! Chagua neno zima kwa mpigo. (Acha kuburuta mouse kuchagua maneno, unajichosha).
Shift + Home: Chagua kuanzia hapo ulipo mpaka mwanzo wa mstari.
Shift + End: Chagua kuanzia hapo ulipo mpaka mwisho wa mstari.
Ctrl + Backspace: Futa neno zima lililopo kushoto (Hii ni tamu sana ukikosea neno refu. Futa lote "pwaa!" mara moja).
Ctrl + Delete: Futa neno zima lililopo kulia kwa kishale.
SEHEMU YA 7: File Management.
Desktop yako imejaa uchafu mpaka wallpaper haionekani? Tumia hizi shortcuts kupanga ma-file yako kijanja.
Ctrl + Shift + N: Create New Folder (Tengeneza folder jipya fasta. Acha Right Click > New > Folder... huo ni uzembe!).
Ctrl + Shift + 3: Icon zinakua ndogo inapendeza sana.
F2: Rename (Chagua file au folder, bonyeza F2, andika jina jipya. Simple).
Alt + Enter: Properties (Unataka kujua hiyo video ina ukubwa gani au Flash imejaa? Chagua file kisha piga hii shortcut).
Ctrl + F (kwenye File Explorer): Search Box (Ruka kwenye kiboksi cha kutafuta file uliyopoteza).
Alt + Up Arrow: Go Up One Level (Rudi kwenye folder la nyuma/mama).
Alt + Left Arrow: Back (Rudi ulikotoka).
SEHEMU YA 8: The "Boss Mode" (Virtual Desktops)
Hii ni kwa wajanja tu. Unataka kufanya kazi, lakini pia unataka kucheki movie au mpira kimya kimya? Tumia Virtual Desktops.
Win + Ctrl + D: Create New Virtual Desktop (Tengeneza desktop mpya safi kabisa. Hapa unaweza kufungua Excel ya kazi, kule nyingine ukafungua YouTube).
Win + Ctrl + Left/Right Arrow: Switch Desktops (Hama kati ya desktop ya kazi na ile ya starehe. Boss akipita, unahamia kwenye kazi "voooop!" kama uchawi).
Win + Ctrl + F4: Close Current Desktop (Funga desktop uliyopo. Hakikisha umehamisha vitu vya maana kwanza).
Win + Tab: Task View (Inakuonyesha desktops zote ulizonazo na windows zote zilizowazi).
SEHEMU YA 9: Browser Tabs Master (Wazee wa Chrome & Edge)
Tunaongezea maujanja ya mtandaoni kidogo kwa sababu tunajua ndio mnaposhinda.
Ctrl + 1 mpaka 8: Switch Tabs (Ruka kwenye tab ya kwanza, ya pili, nk. bila mouse).
Ctrl + 9: Jump to Last Tab (Nenda kwenye tab ya mwisho kabisa kule kulia).
Ctrl + Shift + Delete: Clear Browsing Data (Unataka kufuta ushahidi fasta? Hii inakupeleka kwenye menyu ya kufuta history).
Ctrl + Enter: Auto-complete .com (Andika "facebook" kwenye address bar kisha piga Ctrl+Enter, itajaza yenyewe "www." na ".com". Acha kuchosha vidole).
Spacebar (kwenye YouTube): Pause/Play (Simamisha video).
F (kwenye YouTube): Full Screen (Jaza kioo).
Esc (kwenye YouTube): Exit Full Screen (Toka kwenye kioo kikubwa).
SEHEMU YA 10: The Function Keys (Vitufe Vilivyosahaulika)
Hivi vitufe F1 mpaka F12 juu ya keyboard sio mapambo. Kila kimoja kina kazi yake.
F1: Help (Unakwama? Hii inafungua msaada, japo wabongo huwa hatisomi help π).
F3: Search (Tafuta faili au neno).
F5: Refresh (Iamshe PC au browser iliyolala).
F6: Cycle through screen elements (Inarukaruka kwenye menu mbalimbali za window bila mouse).
F11: Full Screen Mode (Kwenye browser, hii inaficha kila kitu juu na chini, unabaki na website tu. Bonyeza tena kurudisha).
Alt + Print Screen: Screenshot Active Window Only (Piga picha window unayoitumia tu, sio screen nzima na taskbar).
Hitimisho la Part 2
Mwanangu wa 246 Online, ukichanganya shortcuts za Part 1 (1-57) na hizi za Part 2 (58-92), tayari unakaribia mia moja!
Hivi unajua ukiweza kutumia Ctrl + Backspace kufuta maneno na Win + Ctrl + Arrows kubadili desktop, utaonekana kama IT Manager ofisini kwako? Watu watakuheshimu!
Kazi bado mbichi. Kwenye Part 3, tutamalizia zile shortcuts za Advanced System Commands, CMD (Hacker Style), na shortcuts maalum za Windows 11 mpya.
Zoezi la Wiki:
Jaribu kutumia Ctrl + Shift + Arrows kuchagua maandishi unapotype text message au email. Acha kutumia mouse kuburuta!
Tukutane Part 3!
Imeandaliwa na: Team ya Ufundi, 246 Online. (Tunakupa maujanja, wewe kazi yako ni kutoboa!)
Bonyeza icon ya facebook, WhatsApp au mtandao unaotumia ili ku-share na rafiki.

Maoni