246
ONLINE
INITIALIZING
LIVE
Inapakia makala... 246 ONLINE — Intelligence and Information First
Jinsi ya Kufanya Android Yako Iwe na Kasi Balaa (Mara 2 Zaidi) Bila Ku-Format Wala Kutumia App Yoyote! πŸš€Washa "NITROUS" Kwenye Simu Yako: πŸ’¨βš‘
Simon Guyashi
Simon Guyashi
Mwandishi — 246 ONLINE
April 06, 2026
⏱ ...

Jinsi ya Kufanya Android Yako Iwe na Kasi Balaa (Mara 2 Zaidi) Bila Ku-Format Wala Kutumia App Yoyote! πŸš€Washa "NITROUS" Kwenye Simu Yako: πŸ’¨⚡

 Wanangu wa 246 Online, Leo tunaweka injini ya Ferrari kwenye Vitz! 🏎️

Unajua kwanini simu za iPhone zinaonekana zina kasi sana kuliko Android nyingi? Sio kwamba zina RAM kubwa sana, lah. Ni kwa sababu "Animations" zao (jinsi apps zinavyofunguka na kufunga) zimetengenezwa kiufundi sana.

Kwenye Android, makampuni yanaweka "Animations" ndefu na za polepole ili simu ionekane "Smooth", lakini matokeo yake inafanya simu ionekane nzito na inayochelewa.

Leo nakupeleka jikoni ukafanye kitu kinaitwa "SPEED TWEAK". Tunakwenda kupunguza muda ambao simu inapoteza kwenye urembo wa kufungua apps, ili ifungue mambo chapu chapu!


πŸ› ️ Hatua ya 1: Washa Mode ya Ufundi (Developer Options)

Kama kawaida yetu, mambo makubwa hayakai hadharani. (Kama tayari umeshawahi kuwasha hii, ruka hatua hii).

  1. Nenda Settings > About Phone.
  2. Tafuta Build Number na uigongegonge haraka haraka mara 7 mpaka uone maandishi "You are now a developer!".

πŸš€ Hatua ya 2: Weka Nitrous (The Speed Hack)

Hapa ndipo penyewe. Fuata kwa umakini, usibadili kitu kingine nisichosema.

  1. Nenda Settings > System > Developer Options. (Kwenye simu zingine ipo chini ya "Additional Settings").
  2. Shuka chini (scroll) taratibu. Usikimbie. Unatafuta kipengele kinaitwa "DRAWING".
  3. Chini ya "Drawing", utaona machaguo matatu muhimu sana:
    • Window animation scale (Ipo 1x)
    • Transition animation scale (Ipo 1x)
    • Animator duration scale (Ipo 1x)
  4. KAZI YAKO: Bonyeza kila moja wapo, na ubadilishe kutoka "Animation scale 1x" iwe "Animation scale .5x" (Hiyo ni nukta tano x).

BADILISHA ZOTE TATU ZIWE .5x

(Pro Tip: Ukiweka "Animation off" simu itakuwa na kasi ya ajabu lakini itakuwa haina urembo kabisa, itakuwa inakata-kata. Option bora zaidi ni .5x - Kasi na Urembo kidogo).

🏁 Matokeo (The Aftermath)

Ukishamaliza tu kuweka .5x kwenye zote tatu:

  • Bonyeza kitufe cha "Home" kurudi mwanzo.
  • Jaribu kufungua WhatsApp... PAAP! Imefunguka.
  • Jaribu kufungua Settings... PAAP! Imefunguka.
  • Jaribu ku-minimize apps... Zinateleza kama sabuni!

Simu yako sasa hivi inajibu amri zako kwa kasi ambayo hukuwahi kuiona tangu uinunue. Hii ndio inaitwa SPEED DEMON MODE.


Hitimisho: Usiache simu ikupotezee muda wako. Muda ni mali. Kwa tweak hii ndogo, unaokoa sekunde nyingi sana kila siku. Simu inakuwa nyepesi na inafurahisha kuitumia.

Jaribu sasa hivi, alafu rudi hapa uniambie kama hujahisi tofauti!

ENDELEA NA BLOG YETU.

TU-FOLLOW BOFYA HAPA.

#246Online #SpeedHack #AndroidTricks #FasterPhone #DeveloperOptions #Maujanja #NoLag

Soma Pia Hizi
Maoni
0
Anonymous inaruhusiwa — hakuna lazima ya akaunti.
246