246
ONLINE
INITIALIZING
LIVE
Inapakia makala... 246 ONLINE — Intelligence and Information First
Jinsi ya Ku-Install Windows 98 au XP Ndani ya Simu ya Android na Kuigeuza Kuwa Kompyuta Kamili (Cheza Games za PC!)
Simon Guyashi
Simon Guyashi
Mwandishi — 246 ONLINE
May 01, 2026
⏱ ...

Habari mwana 246 Online!

Umewahi kuwaza, hivi inawezekana kubeba Kompyuta nzima mfukoni mwako? Simaanishi kununua Laptop ndogo, namaanisha kutumia simu yako hii hii ya mkononi kufungua Windows!

Fikiria umekaa na washkaji, unatoa simu yako, inawaka, na badala ya kuona Android, inaandika maneno ya BIOS na kutokea logo ya Windows 98 au Windows XP ikiwa na ile sauti yake maarufu Tadaaa! πŸ–₯️πŸ”Š

Huu sio uchawi, wala sio "Theme" au "Launcher" ya kupamba simu. Hii ni EMULATION. Tunatumia nguvu ya simu yako kuendesha mfumo wa kompyuta (Operating System) mzima. Unaweza kutumia Mouse, kuandika kwenye Notepad, na kucheza games za zamani za PC kama Age of Empires, Doom, au Minesweeper.

Leo 246 Online tunakupa mwongozo wa kutumia "Limbo PC Emulator". Twende tukaweke Windows... πŸ’ΏπŸ“±


MAHITAJI (Vifaa Vya Kazi)

Kabla hatujaanza, hakikisha una vitu hivi viwili muhimu:

  1. Limbo PC Emulator: Hii ndio App (Engine) itakayoendesha Windows.
  2. Windows Image File (.img au .iso): Hili ndio faili la Windows lenyewe. (Tunashauri kuanza na Windows 98 maana ni nyepesi na inakubali kwenye simu zote).

HATUA YA 1: Pakua App na File la Windows

  1. Ingia Google, tafuta na upakue "Limbo PC Emulator APK". (Tafuta toleo la karibuni, mfano v5.1.0). Install kwenye simu.
  2. Rudi Google, tafuta faili la Windows. Andika: "Windows 98 img for Limbo emulator download".
    • Ujanja: Tafuta faili dogo (Lite version), linaweza kuwa na MB 200 mpaka 500. Ukilipata, lihifadhi sehemu unayoikumbuka (mfano folder la Downloads).

HATUA YA 2: Set Mitambo (Configuration) ⚙️

Hapa ndipo penye ufundi. Fungua App ya Limbo na ufuate setting hizi kwa umakini ili simu isistaki:

  • Load Machine: Bonyeza New, na uipe jina (mfano: "My Windows 98").
  • User Interface: Chagua SDL.
  • CPU/Board:
    • Architecture: x86
    • Machine Type: PC
    • CPU Model: qemu32 (au Pentium 2).
    • CPU Cores: 1 (Windows za zamani zinataka core 1 tu).
    • RAM: Weka 64MB au 128MB (Usiweke nyingi sana, Windows 98 haihitaji RAM ya GB!).
  • Storage (Hard Disk):

    • Bonyeza kwenye Hard Disk A.
    • Chagua Open.
    • Nenda kwenye mafaili yako na uchague lile faili la Windows 98 (.img) ulilopakua.
  • Graphics/VGA: Chagua Cirrus au Vmware.
  • Boot Settings: Chagua Boot from Hard Disk.

HATUA YA 3: Washa Mashine! (Booting) πŸš€

Ukishamaliza kuseti hizo namba hapo juu:

  1. Bonyeza kitufe cha PLAY (Pembetatu) kilicho juu.
  2. Simu itabadilika screen. Utaona maandishi meusi na meupe ya Bios yakikimbia.
  3. Subiri kidogo... (Inaweza kuchukua dakika 1 au 2).
  4. MAAJABU: Utaona Logo ya Windows inatokea, na Desktop itafunguka!

JINSI YA KUTUMIA (Mouse & Keyboard)

  • Mouse: Tumia kidole chako kuki-slide kwenye kioo cha simu, mshale (Cursor) utatembea. Kugonga mara moja ni Click, kugonga mara mbili ni Double Click.
  • Keyboard: Ukihitaji kuandika, bonyeza icon ya keyboard juu ya screen.
  • External: Kwa uzoefu bora zaidi, chomeka Mouse na Keyboard halisi kwa kutumia OTG (kama tulivyofundisha kwenye post iliyopita), utahisi unatumia kompyuta ndogo kweli!

NINI UNAWEZA KUFANYA?

Sasa unayo PC mkononi:

  1. Fungua Paint uchore picha.
  2. Fungua Notepad uandike siri zako.
  3. Cheza Minesweeper au Solitaire.
  4. Kama wewe ni mbabe, install games za zamani (Retro PC Games) ucheze.

HITIMISHO

Hii project ni ya kibabe sana kwa ajili ya kuonyesha uwezo wa simu yako ("Flexing"). Simu yako sio ya kupigia simu tu, ni mashine!

Jaribu kuweka Windows 98 kwanza uone inavyokimbia. Ukizoea, jaribu kupandisha uweke Windows XP (ila hii inahitaji simu yenye RAM kubwa kidogo).

Tuambie kwenye comments, umefanikiwa kuwasha?

OUR BLOG

Soma Pia Hizi
Maoni
0
Anonymous inaruhusiwa — hakuna lazima ya akaunti.
246