Wanangu wa 246 Online, Leo tunavunja kabati la mafundi! π ️
Kuna vitu kwenye simu yako vimefichwa. Kampuni za simu hawataki uwe unavijua kwa sababu wanataka uwe mtumiaji wa kawaida tu. Lakini hapa 246 Online, tunataka uwe Master.
Leo nakupa Secret Code (Kodi ya Siri) moja ambayo ina kazi mbili nzito sana. Kodi yenyewe ni:
*#*#4636#*#*
(Andika hiyo kwenye sehemu ya kupigia simu, ukimaliza tu nyota ya mwisho, menu ya siri itafunguka).
Hii menu inaitwa "Testing" au "Engineering Mode". Hapa kuna maujanja mawili ya kufanya:
π 1. Lazimisha Internet Iwe 4G au 5G Tu (Force LTE)
Unakuta uko sehemu mtandao unasumbua, simu inahama hama kutoka 4G kwenda 3G au H+. Hii inakera sana ukiwa unadownload au kuangalia YouTube/TikTok. Internet inakuwa konokono.
Jinsi ya Kutibu:
Piga hiyo kodi
*#*#4636#*#*.Ingia "Phone Information".
Shuka chini palipoandikwa "Set Preferred Network Type".
Kwenye list, chagua "LTE Only" (Kwa 4G) au "NR Only" (Kwa 5G).
Matokeo: Simu yako itaganda kwenye 4G/5G kwa nguvu. Haitashuka kwenye 3G kamwe. Internet itapepea kama ndege! (Tahadhari: Ukiweka LTE Only, baadhi ya simu haziwezi kupokea simu za kawaida. Ukimaliza internet yako, kumbuka kurudisha setting iwe "LTE/WCDMA/GSM auto").
π΅️♂️ 2. Mshike Mchawi: Jua Nani Kachezea Simu Yako
Umeacha simu mezani, umerudi unakuta ina joto. Unamuuliza mshkaji/demu wako "Umeishika simu yangu?"anakataa. Anaonesha "Recent Apps" ziko tupu (amezifuta/clear).
Usimbishi. Tumia akili.
Jinsi ya Kumkamata:
Piga hiyo kodi
*#*#4636#*#*.Chagua "Usage Statistics" (Takwimu za Matumizi).
Hapo utaona list ya Apps zote zilizofunguliwa, Muda zilipofunguliwa, na Zilitumika kwa muda gani.
Matokeo: Hata kama alifuta history, hapa haifutiki! Utaona kabisa: "WhatsApp: Last time used 10:15 AM - Duration 5 mins". Unamwambia, "Sasa mbona hapa inaonesha saa nne na robo ulifungua WhatsApp?" Hawezi kuchomoka. π
π Neno la Mwisho
Hii ndio tofauti ya kuwa na simu janja na kuwa mjanja wa simu. Jaribu hiyo kodi sasa hivi uone kama inakubali kwenye simu yako (Inakubali kwenye 90% ya Androids zote ikiwemo Samsung, Tecno, Infinix, Xiaomi).
Kama imekubali, dondosha comment "IMETIKI" hapo chini! π
#246Online #PhoneHacks #AndroidSecrets #Force4G #UjanjaWaSimu
Maoni