Habari Mkuu wa 246 Online!
Moyo unadunda PAAP! Simu yako imeteleza na kudumbukia kwenye sinki, ndoo ya maji, au umenyeshewa na mvua kubwa na sasa spika inatoa sauti kama imebanwa pua (Ghororo). 😱
Kitu cha kwanza kinachokujia kichwani ni: "Niweke kwenye Mchele!"
ACHA MARA MOJA! Huo ni uongo wa zamani. Mchele una vumbi la wanga (starch) ambalo linaweza kuingia kwenye tundu za simu na kuganda humo, ukaharibu simu zaidi. Pia mchele unachukua masaa 24 kukauka, muda ambao maji yanazidi kutafuna motherboard.
Leo 246 Online tunakupa CODE YA KISAYANSI. Tunakufundisha jinsi ya kutumia "Frequency" maalum ya sauti ambayo ikilia, inasukuma maji yote yaliyojificha kwenye spika yatoke nje yenyewe kama yanafukuzwa.
Huu sio uchawi, ni teknolojia. Okoa simu yako sasa hivi... 💧🔊
HATUA YA 1: Fanya Huduma ya Kwanza Chap!
Kabla ya kutumia hiyo sauti:
- Kausha simu kwa kitambaa kikavu kwa nje.
- USICHOMEKE CHAJI! (Hii ni hatari, unaweza kuunguza IC).
- Kama simu imezimika, usi iwashe. Lakini kama inawaka na tatizo ni spika inatoa sauti mbaya, endelea na hatua inayofuata.
HATUA YA 2: Tembelea Tovuti ya "Fix My Speakers"
Hapa ndipo penye dawa.
- Ingia Google Chrome au Browser yoyote.
- Andika:
fixmyspeakers.com - Utaona kitufe kikubwa cheupe chenye picha ya matone ya maji na upepo 💨💧.
(Au unaweza kuingia YouTube na kusearch "Sound to remove water from phone speaker").
HATUA YA 3: Washa Sauti ya Maajabu (The Magic Sound)
- Ongeza Sauti ya simu yako (Volume) iwe MWISHO (MAX). Lazima iwe juu kabisa ili mtetemo uwe mkubwa.
- Bonyeza kile kitufe kwenye hiyo website.
- Utasikia sauti ya ajabu inalia kama ving'ora au Bzzzzzzzz nzito.
HATUA YA 4: Angalia Maajabu!
Wakati sauti hiyo inalia:
- Shika simu yako wima.
- Angalia kwenye matundu ya spika (chini au juu).
- UTASHANGAA: Utaona matone ya maji yakiruka kutoka ndani ya spika na kumwagika nje!
Sauti hii imetengenezwa kwa Frequency ya 165Hz ambayo inatetemesha spika kwa nguvu kiasi kwamba maji hayawezi kukaa ndani. Ni kama vile unavyokung'uta zulia ili vumbi litoke, sauti hii inakung'uta spika yako!
Acha ilie kwa sekunde 60 mpaka uone maji hayatokii tena.
⚠️ ONYO: Usitumie 'Dryer' ya Nywele!
Watu wengi hutumia Hair Dryer kukausha simu. KOSA KUBWA!
- Moto wa dryer unayeyusha gundi (glue) inayoshikilia kioo na betri ya simu yako.
- Pia upepo wa dryer unaweza kusukuma maji yaende mbali zaidi ndani ya simu badala ya kuyatoa.
- Tumia njia hii ya Sauti, ni salama 100%.
HITIMISHO
Basi mzee wangu, ukisikia sauti ya spika imerudi kuwa safi (Crystal Clear), ujue umepona gharama ya Fundi Simu.
Hii trick inafanya kazi pia kwenye Saa Janja (Smartwatch) zilizoingia maji.
Okoa simu ya mshkaji wako kwa kushare naye post hii sasa hivi!