0%
HABARI
⟳ Inapakia maujanja...
246
ONLINE
INAINGIA 246...
00 00 00 00 00
MENYU // 246 ONLINE
Nyumbani AI HUB TZ Maujanja Kuhusu Wasiliana Faragha
SYS:ONLINE
SIGNAL
246CORE:v7.0
TZ//DAR
246
246 ONLINE APPSakinisha sasa kupata maujanja zaidi!

MKAMATE MWIZI WA PASSWORD! Jinsi ya Kufanya Simu "Ijipige Picha" (Selfie) na Kukuonyesha Sura ya Mtu Aliyejaribu Kuifungua Kwa Siri

 Habari Mkuu wa 246 Online!

Ushatoka kuoga au kurudi kutoka ofisini ukakuta simu yako ina alama za vidole au unahisi kuna mtu alikuwa anajaribu kubahatisha Password au Pattern yako ili asome meseji zako?

Unabaki unahisi hisi tu, "Atakuwa Juma? Atakuwa Housegirl? Au ni Mke wangu?"

Acha kuhisi! Leo 246 Online tunakupa ulinzi wa Kijasusi. Tunakufundisha kuweka "Mtego wa Picha".

Ukiweka setting hii, yeyote atakayeshika simu yako na kukosea Pattern au Password, simu itampiga picha ya sura yake (Selfie) kimya kimya bila yeye kujua. Ukija kufungua simu, unakuta Gallery imejaa sura za wadukuzi wote! 📸👮‍♂️

Twende tukawatege...




HATUA YA 1: Pakua "Third Eye" (Jicho la Tatu)

Kuna apps chache zinafanya kazi hii, lakini "Third Eye" au "CrookCatcher" ndio kali zaidi. Leo tutatumia Third Eye.

  1. Ingia Play Store.
  2. Tafuta na upakue App inaitwa "Third Eye - Smart Video Recorder" (Au tafuta "Intruder Selfie").
  3. Install na uifungue.

HATUA YA 2: Washa Mtego (Activate)

Ukifungua App:

  1. Itakuomba ruhusa ya kutumia Kamera (ili ipige picha) na ruhusa ya "Draw over other apps". Kubali zote (Allow).
  2. Kitu muhimu zaidi: Itakuomba uwashe "Device Admin App". Hii ni lazima uikubali (Activate) ili iweze kujua pale mtu anapokosea password kwenye lock screen.

HATUA YA 3: Set Idadi ya Majaribio

Kwenye settings za App, utaona kipengele kimeandikwa "Number of unlock attempts".

  • Weka 1 Attempt.
  • Hii inamaanisha mtu akikosea mara moja tu, kamera inapiga kazi! (Picha inapigwa).

HATUA YA 4: Jaribio (The Trap)

Funga simu yako (Lock screen).

  1. Jaribu kuifungua kwa kuweka Pattern au Password ya uongo.
  2. Simu itakataa (Wrong Pattern).
  3. Hapo hapo, kamera ya mbele imeshakupiga picha chap!
  4. Sasa fungua kwa Pattern sahihi.
  5. Utaona Notification kutoka Third Eye inasema: "1 intruder detected".
  6. Fungua hiyo notification, na utakutana na sura yako uliyopigwa muda ule ukikosea!

ZINGATIO: Picha hizi hazionekani kwenye Gallery ya kawaida (ili mwizi asizifute), zinakaa ndani ya App ya Third Eye pekee.


VIPENGELE VYA ZIADA (Pro Features)

  • Last Unlock Time: App hii pia inakuonyesha muda halisi ambao simu ilifunguliwa mara ya mwisho. Kwa hiyo ukikuta simu imefunguliwa saa 8 mchana wakati wewe ulikuwa nje, unajua kuna mtu anaijua password yako!
  • Google Drive Backup: Unaweza kuset picha hizo zitumwe kwenye Email/Google Drive yako. Hii inasaidia hata kama simu imeibiwa, mwizi akikosea password, picha yake inatumwa kwenye email yako. Unampelekea Polisi sura yake ikiwa clear!

Jinsi ya Kuifuta (Uninstall)

Siku ukitaka kuitoa hii App, usikimbilie ku-uninstall kama apps nyingine, itagoma.

  • Lazima uingie ndani ya App kwanza, ubonyeze menu (mistari mitatu), na uchague "Uninstall". Hii ni kwasababu uliipa ulinzi wa "Device Admin".


HITIMISHO

Usimshutumu mtu bure. Weka mtego huu umkamate na ushahidi mkononi. Akibisha unamuonyesha sura yake alivyokumbatana na simu yako.

Hii ndio maana halisi ya Smart Phone.

ENDELEA KUANGALIA CONTENT ZA BLOG YETU BONYEZA HAPA.

Imeandikwa Na
Guyashi 246
🔓 ANGALIA
UDUKUZI
🔓 MAUJANJA

Gundua maujanja yetu bora ya simu, kompyuta na intaneti. Yote bure, yote kwa Kiswahili!

246 Online App

246 ONLINE APP

Sakinisha app yetu bure kupata maujanja haraka bila kufungua browser!

Haraka Zaidi
🔓 Maujanja Mapya
📲 Inaona Offline
🔔 Taarifa Mara Moja

🔒 Salama kabisa — Hakuna data inayochukuliwa