Habari wana 246 Online! Karibuni tena mjengoni.
Imeshawahi kukutokea umekutana na video kali sana YouTube, labda ni muziki mpya, vichekesho, au mafunzo, na unatamani iwe kwenye simu yako (Gallery) ili uiposti WhatsApp Status au uiangalie baadaye bila bando?
Najua kero kubwa ya YouTube ni kwamba ukidownload video, inabaki humo humo kwenye App (Offline viewing). Huwezi kuituma kwa mtu wala kuiweka status. Wengi wanakimbilia kudownload ma-App kama VidMate au SnapTube ambayo mara nyingi hujaza simu virusi au kutafuna 'storage' bure.
Leo 246 Online tunakupa maujanja (Hacks) matata sana. Jinsi ya kushusha mzigo wowote kutoka YouTube kuingia kwenye Gallery ya simu yako au Kompyuta bila kutumia App yoyote. Njia hii ni salama, haraka na bure kabisa!
Twende kazi... π
NJIA YA 1: Maujanja ya "SS" (Hii ndio nyepesi zaidi!)
Hii njia ni ya kishua na wajanja wachache ndio wanaijua. Huna haja ya kukopi link, unabadili tu herufi kidogo.
Hatua 1: Fungua YouTube kupitia Browser yako (kama Chrome, Opera, au Safari). Usitumie App ya YouTube kwa njia hii. Tafuta video unayotaka.
Hatua 2:
Nenda kwenye sehemu ya anwani (URL) juu kabisa.
Mfano link inaweza kusomeka hivi:
www.youtube.com/watch?v=xyz...
Hatua 3:
Futa sehemu iliyoandikwa ube na . (dot) au ondoa www. na uandike ss kabla ya neno youtube.
Yaani link isomeke hivi:
www.ssyoutube.com/watch?v=xyz...
Kisha bonyeza Enter au Go.
Hatua 4: Utapelekwa moja kwa moja kwenye ukurasa wa kudownload. Chagua ubora wa video unaotaka (Mfano: MP4 720p kwa picha angavu) kisha bonyeza Download.
NJIA YA 2: Copy na Paste (Kwa watumiaji wa App ya YouTube)
Kama unatumia App ya YouTube kwenye simu, njia hii inakufaa zaidi.
- Fungua video unayotaka kwenye App ya YouTube.
- Bonyeza kitufe cha Share kisha chagua Copy Link.
- Fungua Browser yako (Chrome au yoyote) na uingie kwenye tovuti inayoitwa Y2Mate.is au SaveFrom.net.
- Paste ile link kwenye kiboksi utakachokiona, kisha subiri kidogo.
- Zitakuja options mbalimbali:
- Ukitaka Wimbo tu (Bila picha): Chagua Audio (MP3).
- Ukitaka Video: Chagua Video (MP4).
⚠️ Angalizo Muhimu (Usipigwe na Matangazo!)
Tovuti hizi za bure mara nyingi zinategemea matangazo ili kujiendesha. Ukibonyeza "Download" na ukaona tab mpya imefunguka ghafla au tangazo linasema "Simu yako ina virusi" - USIBONYEZE KITU!
Hayo ni matangazo tu. Funga hiyo tab ya tangazo (Close tab) na urudi kwenye ukurasa wa kudownload. Mzigo wako utaanza kushuka.
HITIMISHO
Basi mwanangu wa 246 Online, hapo utakuwa umemaliza mchezo. Hakuna haja tena ya kulalamika bando linaisha kwa kurudia kuangalia video YouTube. Shusha mzigo, weka Gallery!
Vipi, umefanikiwa? Kama una swali dondosha comment hapo chini.
π USIPITWE: [Simu za Ajabu Part 2: Tesla Pi - Simu inayochajiwa na Jua ipo hapa! Bonyeza kusoma]
.png)
Maoni