Latest
Inapakia maujanja...
LOADING HACKS..
246
246 ONLINE APP Install sasa kwa maujanja zaidi!

Search

TESLA MODEL Pi: Simu inayotumia Satelaiti na Kuchajiwa na Jua!! Simu za Ajabu Part 2

Kama ulifikiri simu ya Vivo yenye drone tuliyoiangalia kwenye Part 1 ilikuwa ya ajabu, basi bado hujakutana na "Mnyama" huyu anayetarajiwa kutoka kwa tajiri mkubwa duniani, Elon Musk.

Karibu tena 246 Online Site kwenye mwendelezo wa makala zetu za "Simu za Ajabu". Leo tunaichambua Tesla Model Pi 5G - simu ambayo inasemekana itakuja kuua soko la iPhone na Samsung moja kwa moja.

Hii si simu ya kawaida, ni mashine iliyobeba teknolojia ambayo tumeizoea kwenye filamu za Science Fiction tu.

ANGALIZO: Picha za Concept: Hii ni michoro ya kubuni ya jinsi Tesla Model Pi zinavyotarajiwa kuonekana. Si picha rasmi.


Sifa 4 Zinazoifanya Simu Hii Kuwa ya "Ajabu"

Kwanini simu hii inasubiriwa kwa hamu kubwa? Hizi hapa ni sifa zinazotajwa kuwa nayo:

1. Intaneti ya Satelaiti (Starlink Native)

Hii ndiyo sifa inayotisha zaidi. Simu nyingi tunazotumika sasa zinategemea minara ya simu (Towers) ili kupata network. Tesla Model Pi inasemekana kuwa na uwezo wa kuunganisha intaneti moja kwa moja kutoka kwenye Satelaiti za Starlink.

  • Maana yake: Ukiwa msituni, baharini, au hata jangwani ambapo hakuna minara ya Vodacom au Airtel, wewe utakuwa na High Speed Internet.

2. Kuchajiwa na Jua (Solar Charging)

Uchovu wa kutembea na Power Bank unaweza kwisha. Nyuma ya simu hii, inasemekana kutakuwa na tabaka maalum (photochromic coating) lenye uwezo wa kubadilisha mwanga wa jua kuwa chaji.

  • Hii inamaanisha simu yako itakuwa inaji-chaji yenyewe wakati unatembea juani.

3. Kuunganishwa na Ubongo (Neuralink)

Hapa ndipo penyewe! Kampuni ya Elon Musk ya Neuralink inafanya kazi ya kuunganisha ubongo wa binadamu na kompyuta. Kuna uvumi kuwa Tesla Model Pi itakuwa na uwezo wa kuwasiliana na chips za Neuralink.

  • Fikiria kuweza kuandika meseji au kupiga simu kwa kuwaza tu bila kugusa kioo cha simu! Inatisha, lakini ndio teknolojia inakoelekea.

4. Rangi Inayobadilika (Chameleon Design)

Mwili wa simu hii unatarajiwa kuwa na teknolojia ya kubadili rangi kulingana na mazingira (kama kinyonga) au kulingana na hisia zako, jambo ambalo litaifanya iwe simu ya kipekee zaidi kimuonekano.

Je, Simu Hii Ipo Sokoni?

Kama ilivyo kwa Vivo Drone, Tesla Model Pi bado ni dhana (Concept/Rumor). Elon Musk amewahi kukanusha mipango ya kutengeneza simu huko nyuma, akisema Smartphones ni teknolojia ya kizamani. Lakini, wachambuzi wa mambo wanasema kama Apple na Google wataanza kufungia Apps za Twitter (X), Musk atalazimika kutoa simu yake.

Bei Yake Itakuwaje?

Kwa sifa hizi (Satellite, Solar, AI), simu hii haitakuwa ya bei rahisi. Makadirio ya awali yanaonyesha inaweza kuanzia $1,200 hadi $2,500 (Takriban TSh 3,200,000 mpaka TSh 6,700,000).

Hitimisho

Dunia inakwenda kasi sana. Kutoka kwenye simu yenye Drone (Vivo) mpaka simu inayotumia Satelaiti (Tesla). Je, wewe ungependa kumiliki simu ipi kati ya hizi mbili?

Tuachie maoni yako hapo chini! Bonyeza Hiyo button ya facebook au whatsApp ku-share na rafiki zako

[SOMA PART 1 HAPA: VIVO YENYE DRONE]

Maoni

Comment

SYSTEM COMMENT BYPASS

Mfumo wa maoni umekuwa "Isolated" kwa usalama. Bonyeza kitufe hapa chini kufungua sanduku rasmi la maoni.

LATESTπŸ”₯

Contact Form

246

246 CORE

ARCHITECTING THE FUTURE

CEO
CEO & FOUNDER

246 CHIEF TECH

root@246:~$ _
246 Logo

246 ONLINE APP πŸ“±

Install App yetu uingie kwenye mfumo wetu kwa spidi na uwe wa kwanza kupata maujanja!

246 Logo

INSTALL 246 ONLINE πŸ’»

Pakua App yetu kwenye PC au Simu yako uwe wa kwanza kupata maujanja ya kinyama!