Habari Mkuu wa 246 Online!
Kuna kero kubwa kwenye simu za kisasa (Hasa Tecno, Infinix, na Samsung). Unanunua simu unakuta imejaa ma-App ya ajabu ajabu (Palm Store, Hi Browser, Aha Games, Facebook Services) ambayo huyatumii na HAZIFUTIKI.
Ukijaribu kuzifuta (Uninstall), button imefichwa. Unabaki nazo, zinakula RAM yako na kutuma matangazo ya hovyo.
Watu wengi wanajua njia pekee ya kuzitoa ni ku-"Root" simu (kitu ambacho ni hatari na kinaua warranty). SIO KWELI.
Leo 246 Online tunaingia "Jikoni" kabisa kwenye mfumo wa Android. Tunatumia LADB (Local ADB Shell). Hii inakupa mamlaka ya "Super User" kuamrisha simu ifute chochote unachotaka kwa kutumia Codes.
Hii ni kwa ajili ya wale wenye roho ngumu na wanaojua nini wanafanya. Twende tukaoshe simu... 👨💻⚙️
HATUA YA 1: Washa "Developer Options" & "Wireless Debugging"
Hii inafanya kazi kwenye Android 11 na kupanda juu.
- Nenda Settings > My Phone > Bonyeza Build Number mara 7 mpaka uambiwe "You are now a developer".
- Rudi nyuma, nenda System > Developer Options.
- Shuka chini washa USB Debugging (kwa usalama).
- Muhimu zaidi: Washa Wireless Debugging. (Lazima uwe umeunganishwa kwenye Wi-Fi. Kama huna Wi-Fi, washa Hotspot ya simu nyingine uunganishe).
HATUA YA 2: Pakua "LADB" (Local ADB)
Hii App ndio itatumika kuandika hizo kodi.
- Ipo Play Store (Inauzwa), lakini wewe mjanja unaweza kuipata "toleo la bure" ukigoogle "LADB APK Download".
- Au tumia app mbadala ya bure inaitwa "Brevent".
HATUA YA 3: Unganisha (Pairing)
- Fungua App ya LADB. Itakuomba Port na Pairing Code.
- Nenda kwenye Settings za simu > Developer Options > Wireless Debugging.
- Bonyeza maandishi hayo (usi-switch off), kisha chagua "Pair device with pairing code".
- Utapewa Code (tarakimu 6) na Port (tarakimu 5 za mwisho za IP address).
- Zijaze haraka kwenye App ya LADB na bonyeza OKAY.
- Ikikubali, utaona maandishi mengi yanakimbia (Shell). Upo ndani ya mfumo sasa!
HATUA YA 4: Tafuta Jina la App Unayotaka Kufuta (Package Name)
Huwezi kufuta app kwa jina la kawaida (mfano "Palm Store"). Lazima ujue jina lake la kiserikali (Package Name).
- Pakua app inaitwa "App Inspector" au "Package Name Viewer" Play Store.
- Angalia app unayotaka kuifuta. Mfano Palm Store jina lake linaweza kuwa
com.transsnet.store.
HATUA YA 5: Piga Kodi ya Kufuta (The Kill Command) 💀
Rudi kwenye LADB, na sasa andika kodi hii kwa umakini sana:
pm uninstall -k --user 0 [package_name]
Mfano, kama unataka kufuta Palm Store (com.transsnet.store), utaandika:
👉 pm uninstall -k --user 0 com.transsnet.store
Kisha bonyeza Enter (alama ya mshale/tiki kwenye keyboard).
Ukiona imejibu: Success Basi rudi kwenye menu yako. Utaona ile App IMEPOTEA MAZIMA! Haipo tena. Umeng'oa mzizi.
ORODHA YA APPS ZA KUFUTA (Bloatware List)
Hizi hapa baadhi ya apps zinazokera unazoweza kuzifuta kwa njia hii:
- Chrome:
com.android.chrome(Kama unatumia browser nyingine). - YouTube:
com.google.android.youtube(Kama unatumia YouTube Vanced/ReVanced). - Facebook:
com.facebook.katana - Tecno/Infinix Bloat:
com.transsnet.store,com.transsion.aha.games.
⚠️ ONYO KALI (Disclaimer)
- Usiwe kichaa: Usifute apps ambazo huzijui (kama
com.android.systemuiaucom.mediatek...). Ukifuta apps za mfumo muhimu, simu inaweza kuzima na isiwake tena (Brick) mpaka upeleke kwa fundi Software. - Futa zile unazoziona kwenye menu tu (Apps za User na Apps za Matangazo).
HITIMISHO
Hii ndio inatofautisha "Mtumiaji wa Simu" na "Mtaalam wa Simu". Sasa unamiliki simu yako kwa 100%. Hakuna app itakayokaa kwa lazima.
Hii ni elimu ya juu, itumie kwa umakini!
👉 USIPITWE: [Simu Imekuwa Kompyuta! Jinsi ya ku-install Windows 98 au XP ndani ya simu ya Android na kucheza Games za PC (Limbo x86 Emulator).]