CHAJI INAZINGUA? Jinsi ya Kufanya Simu Ijae Haraka (Fast Charging) Hata Kama Huna Chaja ya 'X2' Wala 'Type-C' ya Bei Mbaya!
Habari Mkuu wa 246 Online!
Unachomeka simu saa 2 usiku ikiwa na 10%, unaamka asubuhi unakuta imejaa 85% tu? Au unachomeka simu ofisini, unakaa masaa mawili imeongezeka asilimia 15%? π€
Hii inakera na inakurudisha nyuma kimaisha. Watu wengi wanakimbilia kununua vichwa vipya vya chaji (vinaandikwa Fast Charging/X2) lakini bado tatizo liko pale pale.
Tatizo linaweza lisiwe chaja, bali ni JINSI UNAVYOCHAJI. Simu ina mambo mengi yanayoendelea kwa nyuma yanayokula umeme wakati unaingia. Ni kama kujaza maji kwenye ndoo huku imetoboka, yanajaa taratibu!
Leo 246 Online tunakupa mbinu 4 za "Kijeshi" za kuifanya simu ijae chapu ndani ya nusu saa. Twende kazi... ⚡π
MBINU 1: Washa "Airplane Mode" (Njia ya Ndege) ✈️
Hii ndio siri kubwa ambayo watu wanaipuuza.
- Sayansi yake: Simu yako inatumia nguvu kubwa sana kutafuta Network (Mtandao), hasa kama eneo hilo mtandao unasumbua. Hiyo process inakula umeme mwingi sana.
- Unachotakiwa kufanya: Ukichomeka tu chaji, shusha pazia la juu na uwashe Airplane Mode.
- Matokeo: Simu itaacha kutafuta mtandao, na umeme wote unaoingia utaenda moja kwa moja kwenye betri bila kupunguzwa. Simu itajaa mara mbili zaidi ya kasi ya kawaida!
MBINU 2: Vua "Kava" la Simu (Phone Case) π₯
Hapa tunacheza na Fizikia ya Joto.
- Betri za simu (Lithium-ion) adui yake mkubwa ni JOTO. Simu ikipata joto wakati inachaji, mfumo wa simu unapunguza kasi ya kuchaji ili isilipuke (Throttling).
- Makava mengi (hasa yale manene ya mpira) yanazuia joto kutoka nje. Hii inafanya simuichemke na kuchaji taratibu.
- Ujanja: Ukichomeka chaji, vua kava uiache simu ipumue. Utaona tofauti kubwa sana ya spidi.
MBINU 3: Usitumie "USB ya Kompyuta"
Kosa kubwa wanalofanya watu ofisini ni kuchomeka waya kwenye Laptop au Desktop ili kuchaji.
- Port za USB za kompyuta zimetengenezwa kusafirisha DATA, sio Umeme. Zinatoa umeme mdogo sana (0.5 Amps), wakati simu inahitaji kuanzia 1.0 au 2.0 Amps.
- Suluhisho: Tumia kichwa cha chaji (Adapter) na uchomeke ukutani (Socket). Ukutani kuna nguvu kamili. USB ya kompyuta tumia dharura tu.
MBINU 4: Safisha Tundu la Chaji (Port Hygiene) π§Ή
Wakati mwingine chaja yako ni nzima, waya ni mpya, lakini simu haijai. Tatizo ni VUMBI.
- Simu inakaa mfukoni, kwenye mkoba, na inakusanya vumbi na nyuzi (lint) ambazo zinaingia na kuganda kule ndani kwenye tundu la kuchajia. Hii inatengeneza "Ukuta" kati ya chaja na simu.
- Ujanja: Zima simu. Chukua kibiriti au kijiti cha meno (toothpick) kikavu, na ukichonge kiwe chembamba sana. Kichokonoe taratibu sana kule ndani kutoa uchafu. Utashangaa unatoa "blanketi" la vumbi!
- Ukichomeka chaji baada ya hapo, itaingia "Gwaaa!" na umeme utatembea.
HITIMISHO
Huna haja ya kununua chaja ya laki moja. Anza na mbinu hizi. Weka Airplane mode, vua kava, chomeka ukutani. Utashangaa "Tecno" yako inajaa kama iPhone 15!
Jaribu leo usiku na uone tofauti.
CONTENT ZA KI-HACKER KILA JUMATATU BOFYA HAPA.
