0%
HABARI
⟳ Inapakia maujanja...
246
ONLINE
INAINGIA 246...
00 00 00 00 00
MENYU // 246 ONLINE
Nyumbani AI HUB TZ Maujanja Kuhusu Wasiliana Faragha
SYS:ONLINE
SIGNAL
246CORE:v7.0
TZ//DAR
246
246 ONLINE APPSakinisha sasa kupata maujanja zaidi!

Jinsi ya Kumfungia Mtu Kwenye App Moja (Screen Pinning) Asiweze Kutoka Wala Kuchungulia Meseji Zako Ukim-azima Simu! 🔒🐭🚫

 Wanangu wa 246 Online, Leo tunawatega wambea! 🕸️

Kuna watu wana tabia mbaya. Unawapa simu waone picha moja, wao wanaanza kusogeza (swipe) kuona nyingine. Unawapa wapige simu, wao wanaingia kusoma meseji.

Huwezi kuwaambia "Usiingie huko" maana utaonekana una siri au unaringa. Dawa yao ni ndogo sana. Inaitwa SCREEN PINNING.

Hii ni feature ya siri ya Android inayokuruhusu ku-lock kioo kibaki kwenye App moja tu. Mtu huyo hawezi kubonyeza "Back", hawezi kubonyeza "Home", wala hawezi kuona Notifications zako. Anakuwa amenaswa!



🛠️ Hatua ya 1: Washa Mitambo (Setup)

Hii ipo kwenye kila simu ya Android (Samsung, Tecno, Infinix, n.k).

  1. Nenda Settings.
  2. Ingia Security (au Password & Security).
  3. Shuka chini kabisa bonyeza Advanced au More Settings.
  4. Tafuta "App Pinning" au "Screen Pinning".
  5. IWASHE (Turn On).
  6. Pia washa kile kipengele cha "Ask for PIN before unpinning" (Hii muhimu sana).

🔒 Hatua ya 2: Mtege Mtu (How to Trap)

Sasa mshkaji amekuomba simu apige, au mtoto anataka kucheza game.

  1. Fungua hiyo App (mfano: Phone ya kupigia).
  2. Bonyeza kitufe cha Recent Apps (kile kitufe cha mraba au mistari mitatu chini kinachoonesha apps zilizofunguliwa).
  3. Juu ya hiyo App, utaona Icon/Logo yake. Bonyeza hiyo Logo.
  4. Kwenye menu itakayotokea, chagua "Pin".

Matokeo: Simu itatoa ujumbe "App Pinned". Mpe simu huyo jamaa. Atapiga simu, akimaliza atajaribu kubonyeza "Back" ili aende WhatsApp... Wapi! Simu haitoki! Atabonyeza Home... Wapi! Atabaki hapo hapo kwenye kupiga simu milele mpaka akurudishie simu akisema "Mwanangu simu yako mbona imeruka network ya touch?" 😂

🔓 Hatua ya 3: Jinsi ya Kujitoa (Unlock)

Amekurudishia simu yako. Ili uitoe kwenye huo mtego:

  1. Bonyeza kwa pamoja kitufe cha Back na Recent Apps (shikilia kwa sekunde 2).
  2. Simu itajifunga (Lock Screen).
  3. Weka Password yako au Fingerprint.
  4. Tayari! Simu imerudi kawaida.

Hitimisho: Hii ni njia ya kijanja na ya kistaarabu ya kulinda siri zako (Gallery/Chats) bila kugombana na watu. Wewe wafungie humo humo wamalize shida zao wakurudishie mzigo wako.

Jaribu sasa hivi ku-pin app moja uone inavyo-stuck!

MAUJANJA ZAIDI HAPA.

#246Online #PrivacyHacks #ScreenPinning #UsiibiweSiri #AndroidTricks #MtegoWaPanya

Imeandikwa Na
Guyashi 246
🔓 ANGALIA
UDUKUZI
🔓 MAUJANJA

Gundua maujanja yetu bora ya simu, kompyuta na intaneti. Yote bure, yote kwa Kiswahili!

246 Online App

246 ONLINE APP

Sakinisha app yetu bure kupata maujanja haraka bila kufungua browser!

Haraka Zaidi
🔓 Maujanja Mapya
📲 Inaona Offline
🔔 Taarifa Mara Moja

🔒 Salama kabisa — Hakuna data inayochukuliwa