0%
HABARI
⟳ Inapakia maujanja...
246
ONLINE
INAINGIA 246...
00 00 00 00 00
MENYU // 246 ONLINE
Nyumbani AI HUB TZ Maujanja Kuhusu Wasiliana Faragha
SYS:ONLINE
SIGNAL
246CORE:v7.0
TZ//DAR
246
246 ONLINE APPSakinisha sasa kupata maujanja zaidi!

Jinsi ya Kuweka Kitufe cha Siri cha "SENSORS OFF" Ili Kuzima Camera, Mic na GPS Zote Kwa Bofyo Moja! (Total Privacy Mode) 🛡️📵🚫

 Wanangu wa 246 Online, Leo tunafunga vioo! 🕶️

Hivi ushawahi kuwaza, ukiwa bafuni au kwenye maongezi ya siri, je, kuna App (kama TikTok, Instagram, au Spyware) inawasha camera au mic yako kukurekodi bila wewe kujua? Kuweka sticker kwenye camera ya mbele ni ushamba.

Leo nakupa ujanja wa Developer Level. Tunakwenda kuongeza kitufe kipya kwenye "Notification Shade" (pale unapowasha Data na Wi-Fi) ambacho ukikibonyeza, Sensors zote za simu zinakufa.

Hata Hacker awe na uwezo gani, hawezi kuwasha camera yako maana umeme wa sensors umekatwa!



🛠️ Hatua ya 1: Ingia Jikoni (Developer Options)

Kama kawaida, lazima uwe Developer kwanza (kama bado hujafanya hivi):

  1. Settings > About Phone.
  2. Gonga Build Number mara 7 mpaka uambiwe "You are now a developer".
  3. Rudi Settings > System > Developer Options.

🎛️ Hatua ya 2: Washa Kitufe cha Siri

Hapa ndipo uchawi ulipo. Fuatilia kwa makini:

  1. Ndani ya Developer Options, shuka chini kidogo tafuta kipengele kimeandikwa "Quick settings developer tiles". (Hii ni menyu ambayo watu 99% hawajawahi kuifungua).
  2. Ukifungua hapo, utaona list ya vitufe. Washa kitufe kilichoandikwa "Sensors Off".

🚫 Hatua ya 3: Jaribu "Blackout"

Sasa toka huko, rudi home screen.

  1. Shusha pazia la juu (Notification Shade) kama unataka kuwasha Data.
  2. Utakuta Kitufe Kipya kimeongezeka kina icon kama ya mapigo ya moyo iliyopigwa mstari. Hiyo ndiyo "Sensors Off".
  3. Bonyeza hicho kitufe kiwake.

Nini Kitatokea?

  • Jaribu kufungua Camera ya simu yako... PAAP! Itagoma kufunguka au itajifunga yenyewe (Security Policy prevents use of Camera).
  • Jaribu kurekodi Voice Note WhatsApp... Wapi! Mic haisikii kitu.
  • Simu yako imekuwa "Bubu na Kipofu".

Matumizi Yake: Washa hiki kitufe ukiwa:

  • Bafuni/Faragha.
  • Kwenye kikao cha siri nzito.
  • Unapohisi unadukuliwa.

Ukitaka kutumia camera tena, shusha pazia, zima hicho kitufe, na maisha yanaendelea!


Hitimisho: Hii ndio inaitwa CONTROL. Usiache simu yako iwe na mamlaka kuliko wewe. Weka hicho kitufe leo uwe unazima "Macho na Masikio" ya simu pale unapojisikia.

Share na washkaji wanaoogopa kurekodiwa buibui!

MAUJANJA ZAIDI KILA JUMATATU BOFYA HAPA.
Kama hutai-follow blog yetu follow.

#246Online #PrivacyHacks #SensorsOff #DeveloperOptions #UsalamaWaSimu #TechBongo

Imeandikwa Na
Guyashi 246
🔓 ANGALIA
UDUKUZI
🔓 MAUJANJA

Gundua maujanja yetu bora ya simu, kompyuta na intaneti. Yote bure, yote kwa Kiswahili!

246 Online App

246 ONLINE APP

Sakinisha app yetu bure kupata maujanja haraka bila kufungua browser!

Haraka Zaidi
🔓 Maujanja Mapya
📲 Inaona Offline
🔔 Taarifa Mara Moja

🔒 Salama kabisa — Hakuna data inayochukuliwa