0%
HABARI
⟳ Inapakia maujanja...
246
ONLINE
INAINGIA 246...
00 00 00 00 00
MENYU // 246 ONLINE
Nyumbani AI HUB TZ Maujanja Kuhusu Wasiliana Faragha
SYS:ONLINE
SIGNAL
246CORE:v7.0
TZ//DAR
246
246 ONLINE APPSakinisha sasa kupata maujanja zaidi!

ULIFUTA PICHA KIMAKOSA? Usilie! Njia Rahisi ya Kurudisha Picha Zilizopotea Kwenye Simu (Hata Kama Ulishafuta Recycle Bin)

 Habari Mkuu wa 246 Online!

Kuna maumivu makali kama kugundua umefuta picha muhimu sana kwenye simu yako kimakosa? Labda ulikua unasafisha simu, au mtoto alichezea simu na kufuta album nzima ya picha za likizo au za ofisini.

Moyo unakwenda mbio, unaangalia kwenye "Trash" au "Recycle Bin" unakuta nako kuko wazi! Unahisi dunia imekuangukia. 😭

Kabla hujakata tamaa, 246 Online tuna habari njema. Picha huwa hazifutiki moja kwa moja kwenye simu (Android) hata kama huzioni. Zinafichwa kwenye kina cha 'Memory' zikisubiri kufutwa kabisa na data mpya.

Leo tunakupa mwongozo wa kutumia "Chimbo" (Recovery Tool) la uhakika kufukua makaburi na kurudisha picha zako zote zilizopotea.

Futa machozi, fuata hatua hizi... 🔍📂



HATUA YA 1: Anza na "Trash Bin" (Wengi Wanasahau Hapa)

Kabla hatujatumia mitambo mizito, hakikisha umekagua sehemu ya kawaida. Simu nyingi za kisasa (Samsung, Tecno, Infinix) zina "Trash Can".

  1. Fungua Gallery au Google Photos.

  2. Nenda kwenye Albums au Library.

  3. Tafuta folder limeandikwa "Trash", "Bin", au "Recently Deleted".

  4. Mara nyingi picha hukaa huko kwa siku 30 kabla ya kufutika jumla. Ikiwepo, ibonyeze na chagua Restore.

Kama haipo huko, basi tatizo ni kubwa. Twende Hatua ya 2. 👇


HATUA YA 2: Pakua "DiskDigger" (Fosholo la Dijitali)

Hii ndio App namba moja duniani kwa kufukua picha kwenye Android bila kuhitaji Kompyuta.

  1. Ingia Play Store.

  2. Tafuta na upakue App inaitwa "DiskDigger Photo Recovery". (Ina icon ya bluu).

  3. Ifungue.


HATUA YA 3: Anza Kuchimba (Scanning)

Ukifungua App, utaona machaguo mawili kulingana na aina ya simu yako:

  • BASIC SCAN (No Root): Hii ni kwa ajili ya simu za kawaida ambazo hazijarootiwa (Simu nyingi zipo hapa).

    • Bonyeza kitufe kikubwa kilichoandikwa "START BASIC PHOTO SCAN".

    • Ruhusu App iingie kwenye ma-file yako (Allow).

App itaanza kuhesabu na kuonyesha picha zilizofutwa. Usishangae ukiona picha za mwaka juzi ambazo ulidhani zilienda na maji!

  • FULL SCAN (Root Required): Hii ni kwa wale wajanja walio-root simu zao. Hii inachimba ndani zaidi na inaweza kurudisha hata video.


HATUA YA 4: Chagua na Okoa (Recover)

DiskDigger itakuletea orodha ndefu ya picha (nyingine zipo, nyingine zilifutwa).

  1. Pitia picha hizo na uweke Tiki (Check) kwenye zile unazotaka kuzirudisha.

  2. Bonyeza kitufe cha RECOVER (Kipo juu).

  3. Itakuuliza unataka kuhifadhi wapi. Chagua chaguo la katikati: "Save the files to a custom location on your device".

  4. Chagua folder lolote (mfano 'Downloads' au 'DCIM') kisha bonyeza OK.

Mchezo umeisha! Picha zako zimerudi kiumeni. ✅


⚠️ Angalizo Muhimu (Pro Tip)

  • Quality: Kwa wale mnaotumia "Basic Scan" (Bila Root), picha zitakazorudi zinaweza kuwa na ubora mdogo kidogo (Low Resolution) kuliko zile za asili. Hii ni kwasababu App inarudisha "Thumbnails". Lakini ni bora nusu shari kuliko shari kamili, sindio?

  • Wahi Mapema: Ukifuta picha, usipige picha mpya au kudownload vitu vingi. Data mpya ikija juu, inafuta kabisa nafasi ya picha za zamani. Fanya recovery haraka!


HITIMISHO

Kupoteza kumbukumbu inauma, lakini teknolojia ipo kukusaidia. DiskDigger ni mkombozi wa wengi.

Kama umefanikiwa kurudisha picha zako, usisahau ku-share post hii na ndugu zako. Huwezi jua nani analia muda huu kisa kapoteza picha za harusi!

👉 USIPITWE: [NAMNA YA KU-SAVE WHATSAPP STATUS]

Imeandikwa Na
Guyashi 246
🔓 ANGALIA
UDUKUZI
🔓 MAUJANJA

Gundua maujanja yetu bora ya simu, kompyuta na intaneti. Yote bure, yote kwa Kiswahili!

246 Online App

246 ONLINE APP

Sakinisha app yetu bure kupata maujanja haraka bila kufungua browser!

Haraka Zaidi
🔓 Maujanja Mapya
📲 Inaona Offline
🔔 Taarifa Mara Moja

🔒 Salama kabisa — Hakuna data inayochukuliwa