Habari Mkuu wa 246 Online!
Unajua kwanini simu za Google Pixel au iPhone zinapiga picha kali sana hata usiku, wakati simu yako yenye "Megapixel 108" inapiga picha zenye ukungu na giza?
Siri sio ukubwa wa lenzi, siri ni Software (Akili ya Kamera). Makampuni makubwa yanatumia Image Processing ya hali ya juu sana kusafisha picha. Simu nyingi za kawaida zina kamera nzuri (hardware), lakini software yake ya kamera (Stock Camera App) ni dhaifu.
Leo 246 Online tunakupa siri ambayo wapiga picha wengi wa Instagram hawasemi. Tunakufundisha jinsi ya kuweka Google Camera (GCam) kwenye simu yako ya Tecno, Infinix, Samsung, au Xiaomi. App hii itailazimisha simu yako kupiga picha kwa Algorithm ya Google Pixel. Utaona tofauti ya mbingu na ardhi, hasa kwenye picha za usiku (Night Mode) na Portrait!
Fanya hivi... 📸✨
HATUA YA 1: Hakiki Kama Simu Yako Inaweza (Compatibility)
GCam haikubali kwenye kila simu kienyeji. Lazima simu yako iwe inaruhusu kitu kinaitwa "Camera2 API".
- Nenda Play Store, pakua app inaitwa "Manual Camera Compatibility".
- Ifungue na bonyeza Start.
- Ikipiga tiki zote za kijani, HONGERA! Simu yako inapokea GCam.
- Ikiwa nyekundu, pole mwanangu, simu yako haiwezi (Mara nyingi simu za 'Android Go Edition' hazikubali).
HATUA YA 2: Tafuta GCam Sahihi ya Simu Yako
GCam haziko Play Store (Hii ni modded app). Lazima uitafute kulingana na toleo la Android yako.
- Ingia kwenye Browser yako (Chrome).
- Andika kwenye Google: "GCam port for [Jina la Simu Yako]".
- Mfano:
GCam port for Tecno Camon 20auGCam for Samsung A14. - Tovuti bora ya kuaminika ni Celso Azevedo au GCam Hub.
- Chagua toleo (Version) linaloendana na Android yako (kama una Android 10, usipakue ya Android 13).
- Download file la .apk.
Kidokezo: Matoleo ya BSG au Shamim mara nyingi yanafanya kazi kwenye simu nyingi.
HATUA YA 3: Install na Uset
- Ukishamaliza kudownload, bonyeza hilo file kulifunga (Install).
- Inaweza kukuomba ruhusa ya "Install from unknown sources", kubali (Allow).
- Fungua App mpya ya Kamera iliyoingia (Itakuwa na icon ya Kamera lakini tofauti kidogo).
Jaribio la Moto (The Test) 🔥
Sasa fanya jaribio.
- Piga picha moja ukitumia kamera yako ya zamani (Stock Cam).
- Piga picha hapo hapo ukitumia GCam mpya.
- Zilinganishe.
Utaona GCam inatoa rangi halisi (Natural colors), inatoa mwanga mzuri kwenye giza (Night Sight), na inatenganisha vizuri mtu na background (Portrait Mode) bila zile bluu-bluu pembeni.
Angalizo
- GCam inatumia nguvu kubwa ya Processor kuchakata picha. Inaweza kuchelewa kidogo (sekunde 2-3) kusave picha baada ya kupiga. Hiyo ni kawaida, inasafisha picha iwe "Kioo".
- Ikigoma kufunguka, jaribu kutafuta toleo jingine (Version) ya chini kidogo.
HITIMISHO
Usinunue simu mpya kisa kamera kabla hujajaribu GCam. Hii ndiyo siri ya wadada wengi wa Instagram unaowaona na picha kali huku wanatumia simu za kawaida.
Umefanikiwa? Tuambie kwenye comment unatumia simu gani na GCam imekubali?
ENDELEA KUKAA NA BLOG YETU, BOFYA HAPA KUPATA MAUJANJA ZAIDI