Habari Mkuu wa 246 Online!
Kuchapa Password au PIN kwenye Kompyuta kila unapoiwasha ni ushamba na inachosha. Mbaya zaidi, unapotype password mbele ya watu, ni rahisi kukukariri.
Laptop za bei mbaya (MacBook au HP Spectre) zinakuja na Fingerprint Scanner. Lakini vipi sisi wenye mashine za kawaida?
Jibu ni SIMU YAKO. Simu yako ya Android tayari ina sensa kali ya Fingerprint. Kwanini usitumie hiyo hiyo kufungua Kompyuta yako?
Leo 246 Online tunakuunganishia mitambo. Utaweza kukaa kitandani, unagusa simu yako Paap! Laptop iliyo mezani inafunguka lock yenyewe.
Twende tukaweke ulinzi wa kidijitali... ππ»
HATUA YA 1: Pakua Programu Kwenye Kompyuta (Windows Module)
Kwanza lazima tufundishe Windows ipokee amri kutoka nje.
- Kwenye Laptop yako, ingia Google na utafute: "Remote Fingerprint Unlock Windows Module" (Angalia link ya XDA Developers au Dropbox inayotolewa na developer Andrew-Darkshaman).
- Pakua faili hilo (mara nyingi ni faili la
.exeau zip). - Install kwenye Kompyuta yako. (Itakuuliza Yes/No, kubali).
- Ukimaliza ku-install, Lock Kompyuta yako (Bonyeza
Windows Key + L). Usiingie ndani bado, baki hapo kwenye Lock Screen.
HATUA YA 2: Pakua App Kwenye Simu
- Chukua simu yako ya Android.
- Ingia Play Store.
- Tafuta na upakue App inaitwa "Remote Fingerprint Unlock" (Ina icon ya Fingerprint ya bluu na kufuli).
HATUA YA 3: Unganisha Simu na PC (Pairing) π
Zingatio: Hakikisha Simu na Kompyuta zimeunganishwa Network moja (Wi-Fi). Kama huna Wi-Fi, washa Hotspot ya simu na uunganishe Laptop hapo.
- Fungua App hiyo kwenye simu.
- Nenda kwenye Menu (mistari mitatu kushoto) > chagua Scan.
- Bonyeza alama ya jumlisha (+) au refresh.
- Jina la Laptop yako litatokea (Desktop-XXXX). Libonyeze na uchague Save.
HATUA YA 4: Weka Password Mara ya Mwisho (My Accounts)
Sasa lazimauipe App ruhusa ya kufungua akaunti yako ya PC.
- Kwenye App hiyo hiyo (kwenye simu), nenda Menu > My Accounts.
- Utaona jina la PC yako likiwa na maandishi mekundu (No accounts selected).
- Bonyeza Add Account.
- Jaza Jina la User wa PC (Username) na Password yako ya PC unayotumia kila siku.
- Scan kidole chako kwenye simu kuthibitisha.
- Maandishi yatabadilika kuwa ya kijani (Selected).
HATUA YA 5: Jaribio (The Magic Moment) ✨
Sasa Kompyuta imejifunga (Lock Screen).
- Usiiguse Kompyuta.
- Fungua App ya Remote Fingerprint Unlock kwenye simu.
- Nenda kipengele cha Unlock.
- Weka kidole chako kwenye sensor ya simu.
- ANGALIA KOMPYUTA: Sekunde hiyo hiyo utaona inafunguka Welcome na kuingia ndani!
Umeua! π
FAIDA ZA HII NJIA
- Usalama: Huna haja ya kutype password mbele ya watu. Unajifanya unachezea simu kumbe unafungua PC.
- Urahisi: Inafunguka haraka sana kuliko kutype.
- Swagga: Ni "Tech Flex" moja matata sana ofisini au chuoni.
HITIMISHO
Fanya maisha yako kuwa rahisi. Unganisha vifaa vyako vifanye kazi pamoja. Fingerprint moja, vifaa viwili!
Jaribu kuweka setup hii leo, utashangaa jinsi ulivyokuwa unateseka kutype password miaka yote.
Maoni