Wanangu wa 246 Online, Leo tunakuwa Ma-Inspector! 🔍
Mjini shule. Kuna mchezo mchafu unachezwa na baadhi ya wauzaji wa simu. Wanachukua simu iliyotumika, wanaibadilisha "Housing", wanaisafisha, wanaifunga kwenye box jipya na kukuuzia kama "Brand New" kwa bei ya dukani.
Wewe unafika nyumbani unafurahia simu mpya, kumbe unatumia simu ya mwaka 2019 iliyochoka ndani!
Leo nakupa SILAHA. Kabla hujatoa pesa, au kama unataka kujua ukweli kuhusu simu yako sasa hivi, piga kodi hizi.
🛠️ Hack 1: Samsung "Birth Certificate" (Kujua Ilizaliwa Lini)
Wauzaji wengi wanajua kodi za kawaida, lakini hii wengi hawaijui. Hii inakuonesha siku ambayo "Main Board" ya simu iliwashwa kiwandani mara ya kwanza.
Fungua sehemu ya kupigia simu.
Piga:
*#12580*369#Simu itafungua menu fupi yenye maandishi ya kijani.
Angalia kipengele kilichoandikwa "RF Cal".
Utafsiri Matokeo:
Hapo utaona tarehe, mfano: 2023.10.12 (Yaan Mwaka 2023, Mwezi wa 10, Tarehe 12).
Kama umenunua simu leo (2025) na muuzaji anakuambia ni mpya, lakini RF Cal inasoma 2021, jua UMEPIGWA! Hiyo simu imekaa stoo miaka 4 au imetumika. Simu mpya "Fresh from Box" RF Cal yake inatakiwa kuwa ya karibuni (miezi michache nyuma).
🛠️ Hack 2: Xiaomi/Redmi/Tecno Hardware Test (Kujua Kama Imechoka)
Kama unatumia Tecno, Infinix, au Xiaomi, kuna njia ya kujua kama Kioo, Spika, au Touch imewahi kufa au kubadilishwa.
Kwa Xiaomi/Redmi: Nenda Settings > About Phone > Gonga "Kernel Version" mara 5 haraka haraka.
Kwa Tecno/Infinix: Piga
*#90#(kwenye baadhi ya models).
Itakufungulia "CIT Menu". Hapa unaweza kutest kila kitu:
Bonyeza "Touch Sensor": Chora kwenye kioo. Kama kuna sehemu haiitikii, kioo ni feki au kibovu.
Bonyeza "Battery Indicator": Angalia afya ya betri.
🛠️ Hack 3: Imei Check (Kujua Kama ni Feki/Clone)
Hii ni ya mwisho na muhimu.
Piga
*#06#kupata IMEI namba.Copy hiyo namba, nenda Google andika "Imei Check Info".
Ingiza namba hiyo.
Kama simu mkononi ni Samsung S22, lakini kwenye mtandao inasoma "Samsung J7" au "Unknown Device", tupilia mbali! Hiyo ni Clone (Copy).
Hitimisho: Usiingie dukani kinyonge. Kuwa na "Ujanja wa 246 Online". Piga hizo kodi mbele ya muuzaji. Ukiona anaanza kutetemeka au kukuzuia usipige, jua HAPO KUNA UBIZI.
Kagua simu yako sasa hivi, je RF Cal yako inasoma mwaka gani? Ni mpya au ni "Bibi Kiroboto"? 😂
Tupe majibu kwenye comments!
#246Online #FakePhoneCheck #SecretCodes #SamsungTips #TechBongo #Usiibiwe