Wanangu wa 246 Online, Kero imeisha leo! 🛑
Hakuna kitu kinaboa kama unacheza game tamu, au unaangalia video kwenye player, ghafla "Paap!" tangazo la betting linatokea na hauwezi kuliruka (un-skippable).
Watu wengi wanadownload ma-App ya ajabu ajabu kuzuia matangazo (AdBlockers) ambayo yanakula chaji na kuifanya simu iwe nzito.
Leo nakupa Ujanja wa DNS. Hii ni kodi ndogo unaiweka kwenye Settings za simu, na simu yako inakuwa "Filter" ya uchafu wote. Matangazo hayawezi kupenya.
🛠️ Hatua kwa Hatua (Dakika 1 Tu)
Hii inafanya kazi kwenye simu zote za Android (kuanzia Android 9 kupanda juu). Fuata hapa:
Nenda Settings.
Ingia Network & Internet (au Connections kama unatumia Samsung).
Shuka chini kabisa utaona pameandikwa "Private DNS".
Kwenye simu nyingi, hii ipo "Off" au "Automatic". Wewe bonyeza "Private DNS provider hostname".
Kwenye mstari wa kuandika, andika maneno haya sawasawa (bila nafasi): 👉
dns.adguard.comBonyeza Save.
🔥 Nini Kitatokea? (The Magic)
Ukishasave tu, utaona kitu cha ajabu:
- Fungua lile Game lililokuwa linakusumbua na matangazo... Kimya! Halileti tangazo lolote.
- Fungua MX Player au app za miziki... Safi! Matangazo ya chini na ya juu yote yamepotea.
- Websites zilizojaa matangazo ya "Virus Alert"... Zimepigwa Lock! Hazifunguki.
⚠️ Angalizo Dogo (Niwe Mkweli)
Hii trick inaondoa matangazo kwenye Apps na Games kwa 90%. Lakini kwa YouTube na Instagram, matangazo bado yanaweza kupita (kwa sababu yale yanatoka server moja na video). Ila kwa kero za kwenye Games na Browsing, hii ni kiboko yao!
Inaokoa bando, inaokoa chaji, na inakupa amani ya moyo.
Hitimisho:
Ujanja sio kuwa na simu kali, ujanja ni kuicontrol simu yako ifanye unachotaka. Weka hiyo dns.adguard.com sasa hivi uone maajabu.
Ukifanikiwa, share hii post na mshkaji wako anayeteseka na matangazo!
ENDELEA KUTUFUATILIA
BOFYA HAPA NAMNA YA KUFICHA PICHA NA MA-FILE YAKO BILA APP YOYOTE.
#246Online #AdBlockHack #AndroidTips #OkoaBando #NoAds #TechBongo
Maoni