💡 Utangulizi:
Simu yako imeanza kuwa nzito au kusumbua? Unabofya app inachukua muda kufunguka? Hakuna haja ya kununua simu mpya — labda unahitaji tu kufanya usafi wa kiteknolojia!
Hizi hapa ni njia 7 za kuongeza kasi ya simu yako, ambazo unaweza kufanya mwenyewe bila mtaalamu wala app za kulipia.
Yaani ni kiboko ya mwendo wa konokono kwenye simu
---
1. 🔄 Futa Cache za Apps
Cache ni data ambazo apps hujaza ili kurahisisha matumizi, lakini zikizidi hufanya simu iwe nzito.
Jinsi ya kufanya (Android):
- Nenda Settings > Apps > Chagua app > Storage > Clear Cache
---
2. 🚫 Ondoa Apps Usizotumia
App nyingi hazifai chochote ila zinatumia RAM na betri. Zifute kabisa au zisimamishe.
Tip: Angalia kwenye Settings > Apps > Installed apps halafu piga “Uninstall” kwa zile za zamani.
---
3. 🎞 Funga Animations (Kwa Speed Boost)
Simu nyingi zina animations ambazo hufanya kila kitu kuchelewa kufunguka.
Jinsi ya kufanya (Android):
- Fungua Developer Options
- Tafuta “Window Animation Scale”
- Punguza hadi 0.5x au uzime kabisa
---
4. 🧹 Safisha File Zilizojirudia (Duplicate Files)
Tumia “Files by Google” au “CCleaner” kufuta picha au video zinazojirudia.
---
5. 🔋 Angalia App Zinazotumia Betri Sana
App zinazotumia betri kwa wingi mara nyingi pia zinachelewesha simu.
Hapa unaweza kuzifuta au kutafuta mbadala wake.
Jinsi ya kuona:
- Settings > Battery > Battery Usage
---
6. ⛔ Zima Background Apps
App nyingi zinaendelea kufanya kazi hata ukiwa huzitumii — hizi hupunguza kasi ya simu.
.jpg)
Tip:
- Nenda Settings > Developer Options > Limit background processes
---
7. 📲 Fanya Restart Mara Moja kwa Wiki
Restart ndogo tu inaweza kusafisha RAM na kuanza upya mfumo wa simu yako. Inasaidia kushangaza sana!
.jpg)
---
✅ Hitimisho:
Usikimbilie kununua simu mpya wakati unaweza kufufua simu yako kwa mbinu rahisi hizi. Jaribu leo moja baada ya nyingine, halafu niambie — simu yako imechange?
---
> Je, ni njia gani uliwahi kujaribu? Tuandikie kwenye comment👇 — na usisahau kushiriki (share) makala hii kwa rafiki anayelalamika kuhusu simu yake!


.jpg)
.jpg)
0 Comments