Habari,
Mimi ni Simon Paul Guyashi, mwanzilishi wa 246 Online. Naandika makala hii kukukaribisha katika ulimwengu mpya wa 246 Online — ikija kisasa zaidi, na ikiwa imeongeza mambo mengi zaidi ya kuzungumzia.

Tunalenga nini sasa?
Hivi sasa 246 Online inalenga makundi matano makuu:
Elimu
Fursa
Ujuzi
Pesa
Tech & AI
Ndani ya kila kategoria kuna vipengele vyake, vilivyolenga kukupa maarifa na huduma bora katika ulimwengu huu wa kidijitali.
Tulipotoka, tunapokwenda
246 Online ilianzishwa mwezi Desemba 2025 ikiwa na mambo ya Tech pekee. Sasa, 246 Online (New Chapter) inakuja na vitu vingine vipya kama 246 Desk, ambayo tutaizungumzia zaidi katika makala zijazo.
Unatafuta makala zilizopita? Makala zote za Tech tulizoandika tangu tulipoanza bado zinapatikana kwenye blogu yetu ya awali.
Natumai utaifurahia safari hii mpya.
Karibu sana.
