0%
HABARI
⟳ Inapakia maujanja...
246
ONLINE
INAINGIA 246...
00 00 00 00 00
MENYU // 246 ONLINE
Nyumbani AI HUB TZ Maujanja Kuhusu Wasiliana Faragha
SYS:ONLINE
SIGNAL
246CORE:v7.0
TZ//DAR
246
246 ONLINE APPSakinisha sasa kupata maujanja zaidi!

Flash au Memory Card Imejaa "Shortcuts"? Usi-Format! Jinsi ya Kuondoa Virusi na Kurudisha File Zako Zote kwa Kutumia CMD (Bila Antivirus)

 Habari Mkuu wa 246 Online!

Imeshawahi kukutokea umechomeka Flash Disk yako ofisini au "Stationery" kutoa copy, uliporudi nyumbani ukakuta ma-file yako yote yamepotea na kumejaa vi-icon vya ajabu (Shortcuts)? 😤

Watu wengi wakiona hivi hupaniki na kuamua ku-Format Flash hiyo, wakidhani vitu vyao vimeliwa na virusi. KOSA KUBWA!

Ukweli ni kwamba, virusi hivyo havijafuta vitu vyako. Vimevificha tu (Hidden) na kuweka hizo shortcuts kama gelesha. Ukiformat ndio unavipoteza mazima.

Leo 246 Online tunakupa maujanja ya Kikompyuta (PC Hack). Tunatumia CMD (Command Prompt) kuamrisha kompyuta iteme vitu vyako vyote vilivyofichwa na kufuta virusi hivyo ndani ya sekunde 30.

Hii ndio njia wanayotumia wataalam wa IT, na leo tunakupa wewe bure. Twende kazi... 💻🛠️




HATUA YA 1: Chomeka Flash na Utambue Jina Lake (Drive Letter)

  1. Chomeka Flash au Memory Card yako kwenye PC.
  2. Fungua "This PC" au "My Computer".
  3. Angalia Flash yako imepewa herufi gani.
    • Mfano: USB Drive (E:) au Removable Disk (F:).
    • Hapa tuchukulie mfano Flash yako ni Disk (G:). (Shika hiyo herufi G).

HATUA YA 2: Fungua Mtambo wa CMD

Hapa ndipo tunapoingiza kodi za kibabe.

  1. Bonyeza kitufe cha Windows kwenye keyboard (kile chenye bendera / vibox).
  2. Andika neno CMD.
  3. Utaona inatokea "Command Prompt". Bonyeza Right-Click juu yake na chagua "Run as Administrator".
  4. Kiboksi cheusi kitafunguka. Usiogope, hapa ndipo jikoni.

HATUA YA 3: Andika Code za Uponyaji

Kwenye kile kiboksi cheusi, fuata hatua hizi kwa umakini:

  1. Andika herufi ya Flash yako ikifuatiwa na nukta mbili.
    • Mfano kama ni G, andika: G: kisha bonyeza Enter.
    • Utaona mstari mpya unaanza na G:\>.
  • Sasa andika code hii ya "Ki-Hacker" jinsi ilivyo (kopi na kupaste au iandike kwa mkono): 👉 EEE

    (Hakikisha umeweka nafasi "space" kama nilivyoweza hapo).

  • Bonyeza Enter.


HATUA YA 4: Subiri na Ushangae

Kompyuta itakaa kimya kwa muda kidogo (kama sekunde 10 au 30 kulingana na ukubwa wa Flash). Ikimaliza, itakulethea mstari mwingine wa G:\>.

Sasa fungua Flash yako kawaida. MAAJABU: Utaona ma-file yako yote (Picha, Music, Documents) yamerudi kama kawaida! Zile Shortcuts zitakuwepo pia, sasa unaweza kuzifuta (Delete) hizo shortcuts tu na kubaki na vitu vyako halisi.


HITIMISHO

Umeokoa kazi zako, picha za harusi, au document za ofisi ambazo ungepoteza kwa ku-format. Hii ndio nguvu ya CMD.

Hii trick inafanya kazi kwenye Flash, External Hard Disk, na Memory Card. Share post hii na mtu ambaye flash yake inasumbua kila siku!

PAGE YETU YA UPDATE ZA HACK KILA JUMATATU BOFYA HAPA.

Imeandikwa Na
Guyashi 246
🔓 ANGALIA
UDUKUZI
🔓 MAUJANJA

Gundua maujanja yetu bora ya simu, kompyuta na intaneti. Yote bure, yote kwa Kiswahili!

246 Online App

246 ONLINE APP

Sakinisha app yetu bure kupata maujanja haraka bila kufungua browser!

Haraka Zaidi
🔓 Maujanja Mapya
📲 Inaona Offline
🔔 Taarifa Mara Moja

🔒 Salama kabisa — Hakuna data inayochukuliwa