Latest
Inapakia maujanja...
LOADING HACKS..
246
246 ONLINE APP Install sasa kwa maujanja zaidi!

Search

INSTABRIDGE PART 02: Kiboko Yake Hii Hapa! (Pata WiFi Passwords Hata Bila MB na Uzione Ulizoconnect) πŸ“ΆπŸ”“

Habari Mkuu wa 246 Online! Kwenye Part 1 tuliona jinsi ya kutumia Instabridge. Lakini kuna changamoto moja: Instabridge inahitaji uwe na internet kwanza ili kutafuta internet. Sasa je, ukiishiwa bando kabisa inakuwaje?

Leo tunakuletea Part 2. Hii ni Advanced Method. Tunatumia App inaitwa WiFi Map na pia tunakupa ujanja wa Kuiba Password ambayo tayari imeunganishwa kwenye simu ya rafiki yako bila yeye kujua.

⚠️ ONYO: Hii ni kwa ajili ya elimu tu (Educational Purpose). Usitumie ujuzi huu kuvunja sheria za nchi.


NJIA YA 1: WiFi Map (Internet ya Bure Offline) 🌍

Hii ndio kiboko ya Instabridge. Uzuri wa WiFi Map ni kwamba inakupa uwezo wa kupakua (Download) ramani nzima ya Tanzania na passwords zake, kisha unazitumia ukiwa Offline (Bila kuwasha data).

Jinsi ya Kutumia:

  1. Download: Ingia Play Store au App Store tafuta "WiFi Map".


  2. Weka Location: Fungua App, chagua mji uliopo (mfano: Dar es Salaam au Mwanza).
  3. Pakua Offline Map: Hapa ndio kwenye ujanja. Nenda kwenye settings za hiyo app, chagua "Download Offline Map". Hii itashusha passwords zote za hoteli, migahawa, na ofisi za karibu kwenye simu yako.
  4. Tumia: Siku ukikwama huna bando, washa location tu, fungua WiFi Map, itakuonyesha wapi kuna WiFi ya bure na password yake ni nini, hata kama huna MB!

NJIA YA 2: Jinsi ya Kuona Password ya WiFi Uliyoconnect (QR Code Trick) πŸ“±πŸ‘€

Umewahi kuunganishwa (connect) kwenye WiFi ya ofisi au ya rafiki yako, halafu ukitaka kumunganisha mwingine unashindwa sababu huni password? Au unataka kujua password ili uiandike pembeni? Tumia hii njia rahisi (Huitaji Root):

  1. Nenda kwenye Settings > Connections > Wi-Fi.
  2. Bonyeza ile alama ya "Gear" (⚙️) au jina la WiFi uliyoconnect.
  3. Angalia chini au pembeni utakuta alama ya QR Code imeandikwa "Share".
  4. Piga Screenshot hiyo QR Code.
  5. Fungua App yoyote ya QR Scanner (au Google Lens ambayo ipo kwenye kila simu ya Android).
  6. Upload hiyo picha ya screenshot.
  7. Boom! πŸ”₯ Itakuonyesha jina la WiFi na Password yake hapo hapo (itaandikwa Pass: xxxxx).

Sasa unaweza kucopy hiyo password na kuitumia kwenye PC au simu nyingine.


HITIMISHO Mambo ni mawili tu mwaka huu: WiFi Map kwa ajili ya kutafuta mpya, na QR Trick kwa ajili ya kuziiba zile ulizopewa. Usisahau kupita kwenye ukurasa wetu wa HACKS kujifunza zaidi.

Tuambie kwenye Comments: Wewe unatumia njia gani kupata bando la bure? πŸ‘‡

Maoni

Comment

SYSTEM COMMENT BYPASS

Mfumo wa maoni umekuwa "Isolated" kwa usalama. Bonyeza kitufe hapa chini kufungua sanduku rasmi la maoni.

LATESTπŸ”₯

Contact Form

246

246 ONLINE

THE FUTURE OF TECH HACKS

CEO
CEO & FOUNDER

246 CHIEF TECH

root@246:~$ _
246 Logo

246 ONLINE APP πŸ“±

Install App yetu uingie kwenye mfumo wetu kwa spidi na uwe wa kwanza kupata maujanja!

246 Logo

INSTALL 246 ONLINE πŸ’»

Pakua App yetu kwenye PC au Simu yako uwe wa kwanza kupata maujanja ya kinyama!